Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:38

Kesi ya washukiwa wa mashambulizi ya 9/11 yaanza tena


Picha ya kuchorwa inayoonyesahali hali ilivyokuwa mahakamani wakati mshukiwa mkuu wa mashambulizi ya 9/11 Kalid Sheik Mohamad alifikishwa mbele ya jaji mwaka wa 2013 katika kambi ya kijeshi ya Guantanamo Bay, Cuba.
Picha ya kuchorwa inayoonyesahali hali ilivyokuwa mahakamani wakati mshukiwa mkuu wa mashambulizi ya 9/11 Kalid Sheik Mohamad alifikishwa mbele ya jaji mwaka wa 2013 katika kambi ya kijeshi ya Guantanamo Bay, Cuba.

Khalid Sheikh Mohammad, kiongozi mwandamizi wa kundi la al-Qaida na anayedaiwa kuwa kiongozi wa mashambulio hayo, anakabiliwa na kesi pamoja na washtakiwa wenzake mbele ya tume ya jeshi katika kambi ya jeshi la Marekani huko Guantanamo Bay, Cuba.

Wanakabiliwa na mashtaka ambayo ni pamoja na kula njama, kushambulia raia, mauaji, utekaji nyara wa ndege na ugaidi. Ikiwa watahukumiwa, wanaweza kupewa adhabu ya kifo.

Mchakato wa kusikilizwa kwa kesi hiyo kwa wale wanaotuhumiwa katika shambulio hilo umekumbwa na changamoto za kisheria kati ya waendesha mashtaka na mawakili wa upande wa utetezi kuhusu ni ushahidi gani unaweza kutumika.

Tofauti hizo zinahusisha masuala yote mawili ya nyenzo zilizoainishwa na utumiaji wa habari iliyopatikana wakati wa mahojiano, ambayo wanasheria wa utetezi wanasema ilipatikana kutokana na kuwatesa washukiwa

Mashambulio hayo yaliwahusisha wanaume kumi na tisa walio na uhusiano na al-Qaida wakiteka nyara ndege nne, na kugongesha mbili kati yazo kwenye majengo ya World Trade Center mjini New York, huku nyingine ikigonga makao makuu ya kijeshi Pentagon, nje kidogo ya Washington.

Ndege ya nne ilianguka katika uwanja katika jimbo la Pennsylvania. Mashambulio hayo yaliwauwa karibu watu 3,000.

Marekani ilijibu kwa kuanzisha uvamizi wa Afghanistan kulenga al-Qaida na kushinikiza Taliban, ambao walishutumiwa kuwapatia hifadhi magaidi, kuwasalimisha

Operesheni za jeshi la Marekani nchini Afghanistan zilidumu kwa miaka 20 tu, zikimalizika mwishoni mwa Agosti wakati Taliban walichukua tena udhibiti wa nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG