Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 11:48

Museveni amlaumu Kagame kwa kufunga mipaka miaka 2 iliyopita


Museveni amkosoa Kagame
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:05 0:00

Museveni amkosoa Kagame

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemlaumu Rais wa Rwanda Paul Kagame  kwa kufunga mipaka baina ya nchi hizo mbili miaka miwili iliyopita.

Pia Museveni amekanusha madai ya Kagame kwamba alikuwa anajionyesha kama mkuu wa eneo hilo.

Museveni ameyasema hayo katika mahojiano maalumu na kituo cha televisheni ya France 24 yenye makao yake nchini Ufaransa.

Pia amekanusha ukosoaji uliotolewa na mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu kama vile Human Rights Watch na Amnesty international, akiyashutumu mataifa yenye nguvu duniani kwa kuingilia siasa za ndani za Uganda.

Museveni alitangaza kwamba uchunguzi dhidi ya mauaji ya zaidi ya waandamanaji 50 wakati wa kampeni za uchaguzi wa rais Novemba mwaka 2020 utawekwa wazi kama ilivyoahidiwa na wale waliohusika watashitakiwa.

Pia amekanusha kuwa alikuwa na hofu na mpinzani wake mkuu Bobi Wine kuwa angeweza kushinda katika uchaguzi. ameongeza kuwa alikuwa tayari kufanya mjadala na mpinzani wake.

XS
SM
MD
LG