Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 23:56

Biden atangaza kanuni mpya za kupambana na Covid


Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Rais wa Marekani Joe Biden Alhamisi jioni amekashifu wanaopinga chanjo ya Covid hapa Marekani, wakati akitangaza kanuni mpya ambazo zinawataka karibu wafanyakazi wote wa serikali kuu kupatiwa chanjo.

Wakati huo huo wamiliki wa makampuni makubwa wameshauriwa kuwapa wafanyakazi wao chanjo pia au kuwafanyia vipimo vya corona kila wiki.

Biden ameamuru wafanyakazi milioni 2.5 wa serikali kuu pamoja na wanakandarasi kwenye mahospitali na vituo vingine vya afya, pamoja na wafanyakazi kwenye makampuni yenye zaidi ya wafanyakazi 100 wapewe chanjo dhidi ya corona, ikiwa juhudi ya kukabiliana na aina mpya ya virusi vya Covid.

Hata hivyo wafanyakazi kwenye makampuni binafsi wanaweza kuamua kupata vipimo vya kila wiki vya corona, badala ya kupokea chanjo kinyume na wafanyakazi wa serikali ambao sasa ni lazima waipokee. Kuna ripoti kwamba baadhi ya makampuni tayari yanashurutisha wafanyakazi wao kupewa chanjo la sivyo wapoteze ajira zao.

Biden wakati akitoa tangazo hilo pia alisema kwamba wizara ya kazi itahitaji makampuni kuwalipa wafanyakazi wake wanaokosa kufika kazini wakati wakienda kupokea chanjo.

Hata hivyo hotuba ya Biden haikufafanua iwapo wafanyakazi wa serikali kuu pamoja na wanakandarasi wanao kataa kupokea chanjo kutokana na sababu za kiafya au kidini watasikilizwa.

Kufikia sasa, zaidi ya wamarekani milioni 177 kati ya jumla ya wamarekani milioni 332 tayari wamepokea chanjo ingawa bado serikali haijaidhinisha chanjo hizo kwa watoto walioko chini ya umri wa miaka 12.

XS
SM
MD
LG