Amesema serikali itaanzisha tena ukuwaji wa uchumi na kutathmini upya mikataba ya uchimbaji madini.
Katika hotuba yake ya kwanza mbele ya bunge tangu ushindi wake mwezi uliyopita, Hichilema amesema maafisa wake watathmini sera za kilimo, kubadili bei za umeme na kufanya mageuzi kwenye kampuni ya taifa ya nguvu za umeme ya Zesco.
Kiongozi huyo amesema juu kwenye agenda yake ni kuujenga upya uchumi wa nchi na kurudisha uaminifu kwenye masoko ya hisa.
Rais Hichilema alisema wameingia madarakani wakikuta hali ya uchumi kuwa mbaya kabisa inayohitaji hatua muhimu na thabiti kuchukuliwa, ili kurudisha pia imani miongoni mwa mataifa fadhili, na kupunguza kabisa matumizi yanayongeza deni la taifa ndani na nje.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la Habari la Reuters