Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:20

Zambia yakabiliwa na ongezeko la maambukizi ya COVID-19


Rais Mteule wa Zambia Hakainde Hichilema
Rais Mteule wa Zambia Hakainde Hichilema

Wakati raia wa Zambia wakiendelea kusheherekea kumalizika kwa uchaguzi mkuu wiki iliyopita, maisha yanaendelea kama kawaida huku kukiwa na ongezeko la wagonjwa wa COVID-19.

Vyombo vya Habari vya Zambia vinaripoti kwamba serikali imewasihi raia wake kuendelea kuchukua tahadhari wakati watu wanaendelea kulazwa hospitali kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Kennedy Malama amesema katika saa 24 zilizopita nchi imerekodi kesi mpya za COVID-19 359 kati ya watu 7,086 waliopimwa.

Dkt Malama amesema kiwango cha vifo kimeongezeka kukiwa na idadi ya vifo vinne vilivyorekodiwa ndani ya saa 24.

Amewataka wananchi kuchukua tahadhari kubwa wakati jopo la ufuatiliaji linaendelea kufanya kazi kudhibiti hali na kutoa tahadhari kwa wale ambao hawafuati masharti ya kujikinga na COVID-19.

Maeneo ambayo yamekumbwa na vifo zaidi ni pamoja na linalozalisha shaba maarufu kama Copperbelt, mashariki mwa Muchinga na majimbo ya kusini.

XS
SM
MD
LG