Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 12:19

Zambia : Kiongozi wa upinzani Hichilema atangazwa mshindi wa urais


Kiongozi wa upinzani Hakainde Hichilema
Kiongozi wa upinzani Hakainde Hichilema

Kiongozi mkuu wa chama cha upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais nchini humo, akishinda zaidi ya asilimia 50 ya kura, akiepuka uchaguzi wa marudio.

Tume ya uchaguzi ya Zambia ilitangaza Jumatatu katika mji mkuu, Lusaka, kwamba Hichilema alikuwa ameshinda kura zaidi ya milioni 2.8, huku Rais wa sasa Edgar Lungu akipata kura milioni 1.8.

Hichilema mwenye umri wa miaka 59, mfanyabiashara tajiri na kiongozi wa Chama cha United Party for National Development amepata ushindi katika jaribio lake la sita kuwania urais.

Ushindi wa Hichilema ulichochewa na kutoridhika kwa wananchi na kuanguka kwa uchumi wa Zambia.

Hali hiyo imesababishwa na kushuka kwa bei ya shaba, biashara yake kuu nje ya nchi na kuongezeka kwa mfumuko wa bei na ukosefu wa ajira, kuwa taifa la kwanza la Kiafrika wakati wa janga la COVID-19 kushindwa kulipa deni kubwa mwaka 2020.

Lungu alishutumu siku ya Jumamosi kuwa uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki baada ya duru ya kwanza ya hesabu ya kura kutolewa, akidai vitendo vya vurugu dhidi ya wafuasi wake na wanachama wa chama chake tawala cha Patriotic Front.

XS
SM
MD
LG