Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:31

Zambia : Upinzani wamshinikiza Rais Lungu kukubali ameshindwa


Rais Edgar Lungu
Rais Edgar Lungu

Rais wa Zambia Edgar Lungu, anazidi kushinikziwa kumtaka akubali kushindwa baada ya wagombea watano wa upinzani, kupinga madai yake kwamba uchaguzi wa rais na wabunge wa Agosti 12, haukuwa huru na wa haki.

Kulingana na gazeti la Nation la Kenya, Rais Lungu mwenye umri wa miaka 64 ambaye anamfuatia mpinzani wake Hakainde Hichilema, katika matokeo yaliyotolewa hadi sasa, hapo Jumamosi, alitoa taarifa ya kushangaza akisema ghasia dhidi ya wafuasi wa chama chake tawala cha Patriotic Front (PF), katika baadhi ya majimbo yalifanya uchaguzi huo usiwe huru na wa haki.

Habari za karibuni zilizotolewa na tume ya uchaguzi Zambia, zilionyesha Hichilema, mfanyabiashara maarufu akiongoza kwa zaidi ya kura milioni moja, dhidi ya Lungu akiwa na kura zaidi ya laki tano.

Viongozi watano wa upinzani, Harry Kalaba, Nevers Mumba, Fred Mmembe, Chishala Kateka, Sean Tembo na Trevor Mwamba, mara moja walimwandikia kiongozi huyo aliyesongwa na matatizo, wakimtaka akubali kushindwa.

XS
SM
MD
LG