Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 11:32

Afrika yapata ushindi katika michuano ya awali ya ndondi kwenye olimpiki


Patrick Chinyemba wa Zambia akishangilia ushindi dhidi ya Alex Winwood wa Australia katika uzani wa Fly
Patrick Chinyemba wa Zambia akishangilia ushindi dhidi ya Alex Winwood wa Australia katika uzani wa Fly

Afrika ilipata ushindi kadhaa wa awali katika mashindano ya ndondi ya  Olimpiki ya Tokyo Jumatatu wakati michezo iliingia wiki yake ya kwanza kamili

Afrika ilipata ushindi kadhaa wa awali katika mashindano ya ndondi ya Olimpiki ya Tokyo Jumatatu wakati michezo iliingia wiki yake ya kwanza kamili lakini pia ilishuhudia bondia mwanamke pekee kutoka Somalia akitolewa kwenye mashindano hayo. Ramla Said Ahmed Ali alipoteza pambano lake la uzani wa Feather kwa pointi 5-0 dhidi ya Maria Claudia Nechita wa Romania wakati bondia mwingine wa kike Khouloud Moulahi Hlimi wa Tunisia alipoteza pia kwa pointi 5-0 dhidi ya Sena Irie wa Japan pia katika uzani wa Feather.

Na kwa upande wa wanaume Tetteh Sulemanu wa Ghana alifuzu kuingia raundi inayofuata baada ya kumshinda Rodrigo de la Rosa Marte wa Jamhuri ya Dominican 3-2 kwa uzani wa Fly, wakati Patrick Chinyemba wa Zambia alimshinda Alex Winwood wa Australia 4-1 pia katika uzani huo huo wa Fly.

Naye Younes Nemouchi wa Algeria alimshinda David Kavuma Ssemujju wa Uganda katika uzani wa kati wakati David Mwenekabwe Tshama wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akimshinda Dieudonne Ntsengue Seyi wa Cameroon 3-2 pia katika uzani huo wa kati. Naye Rajab Otukile Mohammed wa Botswana alishindwa na Martinez Rivas wa Colombia katika uzani wa Fly.

XS
SM
MD
LG