Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 15:42

Samantha Power aahidi kushirikiana na Hichilema katika mapambano ya Covid huko Zambia


Samantha Power, msimamizi wa shirika la Marekani la maendeleo ya kimataifa
Samantha Power, msimamizi wa shirika la Marekani la maendeleo ya kimataifa

Wawili hao walijadili pia mipango ya Hichilema ya kupambana na rushwa  na kuimarisha maadili ya kidemokrasia, uhuru wa vyombo vya habari, na uhuru wa kiraia. Power na Hichilema waliahidi kufanya kazi pamoja, kupambana na janga la COVID-19 na kuharakisha kufufua uchumi wa Zambia

Msimamizi wa shirika la Marekani la maendeleo ya kimataifa, Samantha Power, alimpongeza Hakainde Hichilema hapo Jumanne kwa kuchaguliwa kuwa rais ajaye wa Zambia.

Taarifa iliyotolewa na shirika hilo ilisema Power na Hichilema walijadili jinsi ya uangalizi makini wa asasi za kiraia za Zambia katika mchakato wa uchaguzi, zilivyohakikisha imani kubwa kwa matokeo licha ya vikosi vya serikali kumzuia Hichilema kufanya kampeni katika maeneo kadhaa.

Msemaji alisema kwamba wawili hao walijadili pia mipango ya Hichilema ya kupambana na rushwa na kuimarisha maadili ya kidemokrasia, uhuru wa vyombo vya habari, na uhuru wa kiraia. Power na Hichilema waliahidi kufanya kazi pamoja, kupambana na janga la COVID-19 na kuharakisha kufufua uchumi wa Zambia.

Hakainde Hichilema, Rais mteule wa Zambia
Hakainde Hichilema, Rais mteule wa Zambia

Ushindi wa Hichilema dhidi ya Rais aliyepo madarakani Edgar Lungu katika upigaji kura wa Agosti 12 ulichochewa na kutoridhishwa kwa kiasi kikubwa kuanguka kwa uchumi wa Zambia, ambao umepelekea kushuka kwa bei ya shaba, muuzaji mkuu wa nje, kuongezeka kwa mfumuko wa bei na ukosefu wa ajira.

XS
SM
MD
LG