Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:35

Hichilema aahidi kufufua uchumi wa Zambia


Mshindi wa uchaguzi wa Zambia Hakainde Hichilema muda mfupi baada ya kupiga kura.
Mshindi wa uchaguzi wa Zambia Hakainde Hichilema muda mfupi baada ya kupiga kura.

Baada ya ushindi mkubwa wa kiongozi wa upinzani nchini Zambia, Hakainde Hichilema dhidi ya rais aliyeko madarakani Edgar Lungu, kibarua kikubwa kilichoko sasa ni cha kufufua uchumi wa taifa hilo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Lungu mwenye umri wa miaka 64 alimpongeza Hichilema mwenye umri wa miaka 59 wakati akisema kuwa ataheshimu katiba ili kuhakikisha ubadilishanaji madaraka wenye amani.

Hii ni mara ya tatu kwa chama cha upinzani kuchukua madaraka kwa njia ya amani nchini humo. Hichilema, ambaye alikuwa mkurugenzi mkuu wa kampuni ya hesabu amesema kuwa kipaumbele chake ni kufufua uchumi.

Zambia ni taifa la kwanza kukiri kushindwa kulipa madeni yake ya kimataifa baada ya kutokea kwa janga la corona. Hichilema wakati akihutubia wafuasi wake mjini Lusaka muda mfupi baada ya kupata ushindi alisema kuwa atahakikisha kuwa anatimiza jukumu lake licha ya kuchaguliwa wakati nchi ikiwa katika hali mbaya ya kiuchumi.

Uchumi wa Zambia tayari ulikuwa ukidorora hata kabla ya janga la corona, kutokana na mfumuko wa bei za bidhaa, lakini hali imeharibika zaidi baada ya janga hilo.

XS
SM
MD
LG