Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 03:17

Macron asema jeshi la Ufaransa limemuua kiongozi wa Islamic State


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (Photo by Ludovic MARIN / AFP)
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (Photo by Ludovic MARIN / AFP)

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema Kiongozi wa jihadi wa kundi la Islamic State katika eneo la Sahara ameuawa na jeshi la Ufaransa. 

Macron ameandika katika mtandao wa Twitter na kuelezea kifo cha Adnan Abu Walid al-Sahrawi kama mafanikio makubwa katika vita dhidi ya makundi ya kigaidi kwenye eneo la Sahel.

Adnan Abu Walid al-Sahrawi
Adnan Abu Walid al-Sahrawi

Vikosi vya usalama vya Ufaransa vikiungwa mkono na ujasusi wa Marekani vimekuwa vikiwasaka wana jihadi na maeneo yao kwa miaka mingi.

Makundi ya uasi ya Kiislamu yenye msimamo mkali yameenea kote katika eneo hilo ikiwemo Mali, Niger, Chad na Burkina Faso , na kundi la Islamic State linashutumiwa kufanya mashambulizi mengi katika eneo hilo.

Kiongozi wa Jihad al- Sahrawi alihusika katika mauaji ya wafanyakazi wa msaada wa Ufaransa mwaka 2020.

Alikuwa pia anatafutwa na Marekani kufuatia shambulizi la mwaka 2017 lililosababisha mauaji ya wanajeshi wa Marekani na Niger na ilitoa zawadi ya dola milioni tano kwa taarifa zinazomhusu. Hapo awali alikuwa msemaji wa kundi la waasi la mali la Mujao, kiongozi aliyejitangaza wa kundi la wanamgambo wa al- Mourabitoun.

XS
SM
MD
LG