Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:20

Wanajeshi wa mwisho wa Marekani waondoka Afghanistan


Wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan kwenye picha ya awali
Wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan kwenye picha ya awali

Afisa mmoja wa ngazi ya juu wa Taliban Jumatatu  ameiambia VOA kwamba ndege ya mwisho ya wanajeshi wa Marekani imeondoka kwenye uwanja  wa ndege wa kimtaifa wa Kabul saa sita za usiku kwa saa za huko na kwamba vikosi vyote vya kigeni sasa vimeondoka Afghanistan. 

Tangazo hilo limekuja wakati ikulu ya Marekani pamoja na Pentagon wakiahidi kuendelea kuokoa wamarekani pamoja na watu wa Afghanistan walio hatarini nchini humo, ukisemekana kuwa uokozi mkubwa zaidi uliowahi kufanywa katika historia ya Marekani.

Wakati huo huo baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, Jumatatu limesema kwamba linatumai kwamba Taliban watahakikisha usalama wa watu wanaotaka kuondoka nchini humo.

Kati ya wanachama 15 wa baraza hilo, Russia na China hawakushiriki kwenye rasimu ya azimio hilo lililoandikwa na Marekani, Uingereza na Ufaransa na kuungwa mkono na mataifa mengine wanachama.

Baraza hilo liliangazia taarifa ya Taliban ya Agosti 27 kwamba hawatazuia watu wa Afganistan wanaotaka kuondoka nchini, iwe ni kwa barabara au ndege.

XS
SM
MD
LG