Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 11:40

Viongozi wa mapinduzi ya kijeshi Guinea wawaonya mawaziri


Rais aliyepinduliwa Alpha Conde
Rais aliyepinduliwa Alpha Conde

Wanajeshi waliompindua Rais wa Guinea Alpha Conde wamewaita mawaziri wake na maafisa wa ngazi ya juu wa serikali katika mkutano Jumatatu, siku moja baada ya mapinduzi yaliyo laaniwa kimataifa.

Msemaji wa kikosi cha Jeshi ameiambia televisheni ya taifa kuwa yeyote kati ya mawaziri na maafisa atakaye shindwa kuhudhuria mkutano wa saa 1100 GMT atachukuliwa kuwa ni “muasi.”

Mapinduzi ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi ambayo ina hazina kubwa ya madini aina ya bauxite, ambayo yanatumika kuzalisha chuma aina ya aluminum, imesababisha kupanda kwa bei ya chuma kuwa juu zaidi katika kipindi cha miaka 10 Jumatatu kwa hofu ya kuyumba kwa kupatikana bidhaa hiyo katika masoko madogo. Hakuna ishara zozote za kuyumba kwa bidhaa hiyo hadi sasa.

Harakati zilianza polepole, na baadhi ya maduka yalifunguliwa tena katika eneo la wilaya ya Kaloum mjini Conakry lenye ofisi za utawala ambapo ilishuhudiwa milio mikubwa ya risasi siku yote ya Jumapili wakati vikosi maalum vikipambana na wanajeshi waliokuwa wanamuunga mkono Conde.

Msemaji wa jeshi amesema kupitia televisheni kuwa mipaka ya anga na ardhini imefunguliwa tena.

Hata hivyo, hali ya wasiwasi bado inaendelea. Wakati kikosi maalum kilionekana kumshikilia Conde, kililitangazia taifa hilo la Afrika Maghribi kupitia televisheni ya taifa kuwa wameivunja serikali na katiba, na vitengo vingine vya jeshi bado havijatoa tamko hadharani.

Kikosi hicho maalum kinaongozwa na Afisa wa zamani wa wapiganaji mashujaa wa Ufaransa, Colonel Mamady Doumbouya, aliyesema kupitia televisheni ya taifa Jumapili kuwa “umaskini na ufisadi uliokithiri” ulipelekea majeshi yake kumuondoa Conde madarakani.

Mapinduzi hayo yamelaaniwa na baadhi ya nchi washiriki wakuu wa Guinea. Umoja wa Mataifa mara moja ulilaani mapinduzi hayo, na Umoja wa Afrika na Umoja wa nchi za Afrika Magharibi wametishia kuwawekea vikwazo.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG