Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:06

Tanzania yaanzisha uchunguzi wa tuhuma za ubakaji dhidi ya polisi


Inspekta Jenerali wa Polisi Tanzania, IGP, Simon Sirro
Inspekta Jenerali wa Polisi Tanzania, IGP, Simon Sirro

Polisi Tanzania imesema Ijumaa walikuwa wanachunguza madai dhidi ya baadhi ya maafisa wa polisi kuhusika na ubakaji na udhalilishaji wa kingono wa wanawake kadhaa katika vilabu vya usiku.

Hatua hii ni kufuatia kusambaa madai hayo ambayo yalisababisha malalamiko na wito wa kuchukuliwa hatua za haraka.

Shutuma hizo zimetolewa wakati wa mkutano wa hadhara na kamishna wa polisi wa wilaya ya Handeni, katika mkoa wa Tanga wiki hii.

Ramani ya Tanzania
Ramani ya Tanzania

Video za televisheni za mkusanyiko huo ziliwaonyesha wanawake wakilia wakati wakieleza madhila yaliyo wafika.

“Wanakulazimisha ufanye nao ngono na ukikataa, watatengeneza sababu ambazo sio muhimu za kukukamata na kukuweka rumande,” mwanamke moja, ambaye hakuweza kutambuliwa alisema katika video hiyo.

Wanakuja usiku wa manane na silaha zao na kufanya wanachokitaka kwa wanawake. Ni ukatili mkubwa,” mwanaume mmoja katika mkutano huo amesema.

Wanasiasa wametaka hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya polisi hao waliotajwa katika video hiy0, wakati kitengo cha wanawake cha chama cha upinzani cha Chadema kikiwasihi “wanawake wote wengine wanaokabiliwa na vitendo vya ukatili vya kijinsia kupaza sauti zao.”

“Huu ni udhalilishaji na uhalifu dhidi ya wanawake, unaofanywa na watu ambao walikuwa na wajibu wa kuwalinda wanawake,” chama kingine cha upinzani, ACT Wazalendo kimesema katika taarifa yake.

“Baada ya kuona uovu wa madai haya, tumemtuma afisa wetu kufanya uchunguzi juu ya suala hilo na kufahamu kile hasa kilichotokea,” msemaji wa polisi David Misime amesema katika tamko lake.

“Tunakusanya Ushahidi na tukithibitisha kuwa madai hayo ni kweli, hatua zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria. Hakuna mtu aliyekuwa juu ya sheria,” amesema.

Chanzo cha Habari ni Shirika la habari la AFP na gazeti la The East African, Kenya

XS
SM
MD
LG