Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:20

Kesi ya Mbowe na wenzake imeahirishwa hadi Agosti 13


Freeman Mbowe, kiongozi wa chama cha upinzani CHADEMA nchini Tanzania
Freeman Mbowe, kiongozi wa chama cha upinzani CHADEMA nchini Tanzania

Freeman Mbowe na wenzake wanakabiliwa na tuhuma za ugaidi na walifika mahakamani. Ulinzi ulikuwa mkali sana kwenye mahakama hiiyo na hakuna wafuasi wa Chadema waliofika hapo kama ilivyokuwa Alhamisi

Mwenyekiti wa chama cha upinzani cha CHADEMA nchini Tanzania, Freeman Mbowe kesi yake ya shutuma za ugaidi na biashara haramu ya mzunguko wa fedha iliahirishwa kwa mara nyingine tena katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam baada ya upande wa mashtaka kuieleza mahakama kuwa haujakamilisha baadhi ya mambo ikiwemo taratibu za kufungua kesi ya ugaidi katika mahakama kuu.

Mbowe na wenzake wanakabiliwa na tuhuma za ugaidi na walifika mahakamani. Ulinzi ulikuwa mkali sana kwenye mahakama hiiyo na hakuna wafuasi wa Chadema waliofika hapo kama ilivyokuwa Alhamisi.

Kesi hiyo imeakhirisha hadi wiki ijayo Agosti 13 na Mbowe amerudishwa rumande kwasababu makosa anayotuhumiwa nayo hayana dhamana.

XS
SM
MD
LG