Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 15:29

Jenerali wa Marekani : Afghanistan inaweza kurudi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe


Jenerali Mark Milley (AP Photo/Susan Walsh)
Jenerali Mark Milley (AP Photo/Susan Walsh)

Kuna “uwezekano” wa kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Afghanistan, jenerali wa juu wa Marekani ameviambia vyombo vya habari ya Marekani Jumamosi, akionya kuwa hali hiyo inaweza kurejesha tena vikundi vya kigaidi nchini humo.

Wakati majeshi ya Marekani yalipoanza kuondoka, Taliban walichukua udhibiti wa Afghanistan kwa haraka, ambapo jimbo la kaskazini la Panjshir bado liko chini ya vikundi vya Kiislam venye msimamo mkali.

“Kwa makadirio yangu ya kijeshi… ni kuwa hali hiyo inaweza kupelekea vita vya wenye kwa wenyewe,” Jenerali Mark Milley, mwenyekiti wa wakuu wa majeshi , ameiambia Fox News.

Alihoji iwapo Taliban – ambao bado hawajatangaza serikali – wataweza kuimarisha uongozi wao na kuunda serikali imara.

“Nafikiri angalau kuna fursa nzuri sana uwezekano wa vita vya wenyewe kwa wenyewe na hali hiyo huenda ikapelekea, kwa kweli, kuundwa upya kwa kundi la al-Qaida au kukua kwa ISIS au vingine vya kigaidi,” Milley amesema.

Alisisitiza kuwa hawezi kutabiri kitakachotokea baadae nchini Afghanistan, hata hivyo alitoa tathmini hasi.

“Hali ilivyo inawezekana,” Milley ameiambia Fox News, “unaweza kuona kuzuka tena kwa ugaidi katika eneo hilo kwa ujumla kati ya miezi 12, 24, 36.”

Marekani iliivamia Afghanistan na kuuondoa utawala wa kwanza wa Taliban mwaka 2001 kufuatia mashambulizi ya Septemba 11 yaliyofanywa na al-Qaida, ambao walikuwa na wamepewa hifadhi nchini humo.

Serikali za Magharibi zinahofia Afghanistan inaweza kurejea kuwa maficho ya vikundi vyenye msimamo mkali vinavyo dhamiria kuwashambulia.

Marekani imesema itaendeleza uwezo wa “upeo wake” kushambulia dhidi ya vitisho vyovyote kwa usalama wake huko Afghanistan.

Chanzo cha Habari hii ni shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG