Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 23:48

Watu wa Uyghur wahofia maisha yao Afghanistan


Waandamanaji wa kabila la Uyghur wakiandamana dhidi ya China kwenye picha ya awali
Waandamanaji wa kabila la Uyghur wakiandamana dhidi ya China kwenye picha ya awali

Maisha ya takriban watu 2,000 wa kabila la Uyghur waliozaliwa au kuishi Afghanistan, huenda yakawa hatarini baada ya Taliban kuchukua udhibiti wa taifa hilo, wengi wakihofia kurejeshwa China na kujiunga na wenzao takriban milioni 1 walioko kwenye kambi kwenye jimbo la Xinjiang.  

Idadi hiyo imetolewa na watu wa Uyghuru wanaoishi Afghanistan wakati wakiisimulia VOA kuhusu wasiwasi wao hasa wakati wanapo ona maafisa wa China na Taliban wakiashiria kushirikiana katika siku za nyuma.

Memet ambaye ni mfanyabiashara wa mikufu mjini Kabul kutoka kabila la Uyghur, na ambaye ni baba wa watoto watano,ameiambia VOA kwamba anahofia maisha yake zaidi ya wakati wowote ule.

Anasema kuwa Taliban ambao wanahitaji msaada wa kifedha hawana budi kuwapeleka China ili wapate misaada hiyo. Kulingana na serikali ya China zaidi ya watu milioni 12 kutoka kabila la Uyghur wanaishi kwenye jimbo la Xinjiang, linalopakana na Afghanistan.

XS
SM
MD
LG