Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 23:02

Taliban : Pendekezo la muundo mpya wa serikali Afghanistan utatafuta uhusiano mzuri na Marekani


Mullah Abdul Ghani Baradar, Naibu kiongozi wa Taliban na mwakilishi wa mazungumzo, na wajumbe wengine wakihudhuria mazungumzo ya amani ya Afghanistan Moscow, Russia Machi 18, 2021Alexander Zemlianichenko/Pool via REUTERS/File Photo
Mullah Abdul Ghani Baradar, Naibu kiongozi wa Taliban na mwakilishi wa mazungumzo, na wajumbe wengine wakihudhuria mazungumzo ya amani ya Afghanistan Moscow, Russia Machi 18, 2021Alexander Zemlianichenko/Pool via REUTERS/File Photo

Taliban inakaribia kutangaza pendekezo la kuunda serikali ya Afghanistan, ambayo wanasema itatafuta ushirikiano wa kirafiki wa kidiplomasia na Marekani, na dunia nzima, utakaojikita katika “pande zote kuheshimiana.”

Afisa wa ngazi ya juu wa Taliban, Bilal Karimi, mjumbe wa Tume ya Utamaduni, ameiambia VOA tarehe bado haijapangwa kwa tangazo hilo, lakini itafanyika “mapema sana.” Alikuwa anajibu ripoti za kuwa wanaharakati hao wa Kiislam wanataka kutangaza serikali yao Ijumaa.

Taliban wanafuatiliwa kimataifa kutekeleza ahadi zao kuhusu mfumo wa utawala utakowakilisha makundi yote ya kikabila nchini Afghanistan na kuheshimu haki za binadamu, hususan za wanawake, kinyume na msimamo mkali wa kipekee wa zamani wa utawala huko Kabul.

“Itakuwa inajumuisha serikali kuu yenye nguvu na mifumo endelevu ya serikali. Tayari tuna uhusiano mzuri na nchi nyingi na hatutarajii matatizo yoyote,” Karimi ameiambia VOA alipoulizwa iwapo pendekezo lao la utawala litawasaidia kupata utambuzi wa kimataifa wanaouhitaji sana.

Dominic Raab
Dominic Raab

Uingereza imesisitiza Ijumaa itawataka Taliban kutekeleza ahadi zao, na kuhakikisha kuwa “maneno yao yanaendana na vitendo vyao.”

Akizungumza nchini Pakistan, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Dominic Raab amesema nchi yake ilikuwa inaendelea kufuatilia “ukweli mpya” nchini Afghanistan na haitaki kuona mifumo ya kijamii na kiuchumi ya nchi hiyo ikivunjika.

Mwelekeo tunaochukua, hatuwatambui Taliban kama serikali, lakini tunaona umuhimu wa kuendelea kuwasiliana nao na kuwepo mawasiliano ya moja kwa moja,” Raab amesema.

Mullah Abdul Ghani Baradar,
Mullah Abdul Ghani Baradar,

Karimi amepuuza ripoti za vyombo vya habari “si sahihi”kuwa naibu kisiasa, Mullah Abdul Ghani Baradar, muasisi mwenza wa kikundi hicho, atakuwa kiongozi wa serikali hiyo mpya.

Taliban walikamata udhibiti wa mji mkuu wa Afghanistan mwezi uliopita kufuatia ushindi wa haraka wa kijeshi ulioshangaza, wakichukua udhibiti wa majimbo 33 kati ya 34 katika kipindi cha wiki moja.

Kikundi hicho chenye msimamo mkali kilipata tena madaraka huko Kabul baada ya takriban miaka 20 iliyopita kufuatia uvamizi ulioongozwa na Marekani nchini humo kuwaondoa madarakani kwa kuwapa hifadhi viongozi wa al-Qaida waliolaumiwa kutekeleza mashambulizi ya kigaidi Marekani Septemba 2001.

Marekani na wafadhili wengine wa kimataifa wamesitisha programu za msaada ya kifedha kwa Afghanistan, wakiunganisha kurejeshwa tena kwa misaada kutategemea muundo wa serikali ya siku za usoni ya Taliban.

XS
SM
MD
LG