Polisi walisema mshambuliaji aliyeua kwa risasi maafisa watatu wa polisi na mlinzi mmoja wa kampuni ya kibinasfi katika mtaa wa afisi za balozi jijini Dar Es Salaam mwezi uliopita, alibadilika na kuwa mtu mwenye itikadi kali kwa sababu ya mtandao wa internet.
Lakini ijumaa, gazeti la Raia Mwema lilimuhusisha mtu huyo mwenye silaha kwa jina Hamza Mohamed na Chama Cha Mapinduzi (CCM) cha rais Samia Suluhu Hassan.
Msemaji wa serekali Gerson Msigwa amesema gazeti hilo limesimamishwa kwa sababu ya kuchapisha habari za kupotosha na kukiuka sheria na kanuni za utangazaji.
Amesema “ huo ni ukiukaji wa masharti ya leseni na tishio kwa usalama wa taifa kwa kuandika habari ambazo zinajenga chuki katika jamii.”
Mwezi uliopita, serikali ilisimamisha uchapishaji wa gazeti linalomilikiwa na CCM kwa siku 14, kwa kuchapisha kile ilichokiita “habari ya uongo” kuhusu rais Samia Hassan, habari iliyosema kuwa rais hana nia ya kuwania urais kwenye uchaguzi wa mwaka wa 2025.