“Chanjo hizo zitatolewa na kusambazwa kwa kuzingatia mpango wa Umoja wa Afrika wa upokeaji wa chanjo uitwao AVAT, na ule wa Covax,” taarifa hiyo imeongeza.
Ufaransa ilisema kiasi cha kutosha cha dozi hizo sasa kimenunuliwa kupitia mpango huo wa AVAT, ili kuwezesha watu milioni 400 barani Afrika kupokea chanjo za kujikinga na Covid-19, ambayo ni theluthi moja, ya idadi ya watu barani humo.
Chanjo hizo zitakuwa zimewafikia walengwa wote kufikia Septemba mwaka wa 2022 na zitagharimu dola za Marekani bilioni tatu, taarifa hiyo ilieleza.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, ambaye ndiye mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika ameeleza kuridhika kwake na mpango huo wa utoaji chanjo kwa nchi za bara la Afrika.