Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:18

Jumuiya za kimataifa yazitaka Algeria na Morocco kutafuta suluhu


Ramani ya Morocco na Algeria
Ramani ya Morocco na Algeria

Jumuiya ya nchi za Kiislamu, Umoja wa Nchi za Kiarabu na Ufaransa zimetoa wito kwa Algeria na Morocco kutanzua mvutano kati yao kwa njia ya majadiliano.

Wito huo umetolewa baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria kutangaza Jumanne kwamba nchi yake ina vunja uhusiano na jirani yake Morocco kutokana na vitendo vya uhasama vinavyofanywa na serikali ya Rabat.

Kuna wito wa kimataifa unahimiza kutanzuliwa mivutano ya miezi kadhaa kati ya nchi hizo mbili ya Afrika Kaskazini.

Jumuia ya Nchi za Kisalmu OIC, pamoja na Umoja wa Nchi za Kiarabu, Ufaransa, Saudi Arabia na Libya zilitoa tamko wakati mmoja Jumatano kuzitaka Algeria na Morocco kutafuta njia za majadiliano na kutosababisha mivutano yao kuendelea zaidi.

Wamorocco wengi wamesikitishwa na uamuzi wa Algeria kuvunja uhusiano wao. Salah, mkazi wa Rabat anasema hili ni tatizo kati ya serikali na serikali na wala sio kati ya wananchi, inaripoti Shirika la habari la AFP.

Salah mkazi wa Rabat anasema : "Wananchi wa Morocco na Algeria daima wataendelea kua ndugu, mivutano imebuniwa na serikali na hali hii haitoathiri uhusiano kati ya ndugu wawili. Mivutano hii imekuwepo kwa miaka mingi kati ya nchi zetu mbili."

Waalgeria kwa upande wao wanaunga mkono uamuzi wa serikali yao. Youcef mkazi wa Algiers anasema wamechoshwa na uhasama wa Morocco.

Youcef Mkazi wa Algiers anakaririwa na shirika la havari la Reuters : "Uhasama wao kuelekea Algeria umeongezeka, hivyo Algeria ili bidi kuchukua uwamuzi. Hata hivyo inabidi kwa wananchi kutowafikiria sana maadui tuna bidi kufanya kazi pamoja kwa ajili ya ustawi wa nchi yetu."

Waziri Ramtane Lamamra
Waziri Ramtane Lamamra

Akizungumza na waandishi habari siku ya Jumanne kutangaza uamuzi huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Ramtane Lamamra amesema wanavunja uhusiano kutokana na habari na ukweli wa mambo unaotokana na vitendo mbali mbali vya uhasama vinavyofanywa na nchi jirani.

Waziri Lamamra anasema : "Uamuzi wa kuvunja uhusiano utapelekea kutathmini tena uhusiano wote kati ya nchi zetu na mapendekezo yatakayotolewa kuhusiana na kinachohitajika kufanywa kukabiliana na hali hii mpya yatatekelezwa."

Hatua hii inafuatia kipindi cha kuongezeka kwa mivutano kati ya nchi hizi jirani za Afrika magharibi ambazo tangu mwaka 1975 zimekua zikilaumiana kuhusiana na suala la uhuru wa Sahara ya Magharibi.

Mambo yalizidi kua mabaya wiki chache zilizopita pale rais Abdelmajid Tebboune kutangaza kwamba moto wa msituni ulosababisha vifo vya watu 90 wakiwemo wanajeshi 30 uliwashwa kwa makusudi na ni uhalifu. Na amelituhumu vuguvugu la kupigania uhuru wa jimbo la Kabyle, MAK kuhusika na uhalifu huo na kuituhumu Morocco kukisaidia kubndi hilo.

Hapo tena balozi wa Morocco kwenye Umoja wa Mataifa alisema kwamba wananchi wa jimbo hilo wanastahiki kua na haki ya kuamua mustakbali wake.

Mwezi uliyopita Mfalme Mohamed wa sita wa Moroco alikemya kuzorota uhusiano kati ya nchi zao na kumalika rais Tebboune kwa mazungumzo ya kurudisha uhusiano mzuri kati yao.

Rais Joe Biden
Rais Joe Biden

Lakini mwiba kwenye uhusiano huo ulicoma zaidi pale Israel ilikubaliwa na Umoja wa Afrika kua na kiti cha mfuatiliaji kwenye umoja huo, jambo ambalo Algiers na nchi nyingi za Afrika zimekasirishwa kwa kutoarifiwa kabla. Na vile vile dalili za utawala wa Biden kutokuwa na nia ya kubadili uamuzi wa Trump kuitambua Sahara ya magharibi kama sehemu ya Morocco kumezidisha hasira upande wa Algiers, .

XS
SM
MD
LG