Taarifa iliyotolewa inasema kwamba wale waliokusanyika katika eneo hilo wakitaka kuondoka nchini humo wanapaswa kuhamia eneo salama.
Kwa sababu ya vitisho vya usalama nje ya milango ya uwanja wa ndege wa Kabul, tunashauri raia wa Marekani waepuke kusafiri kwenda uwanja wa ndege.
Pia wametakiwa kuepuka kutumia milango ya uwanja wa ndege wakati huu isipokuwa tu wakipokea maagizo binafsi kutoka kwa mwakilishi wa serikali ya Marekani kufanya hivyo, Ubalozi wa Marekani mjini Kabul ulisema katika taarifa.
Waziri anayehusika na Jeshi la Uingereza James Heappey aliiambia BBC, kwamba kuna ripoti za kuaminika sana kuhusu shambulizi la kigaidi.