Rais Muhammadu Buhari ameonyesha ushawishi kuwa na ushirikiano na Russia tangu mwaka 2019 alipokutana na Rais wa nchi hiyo Vladimir Putin.
Balozi wa Nigeria nchini Russia wakati huo alisema, Buhari anaona Russia inaweza kusaidia kulishinda kundi la Kiislamu la uasi la Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi ambalo bado ni tatizo kubwa.
“Ushirikiano wa kijeshi katika masuala ya kiufundi baina ya nchi zote unatoa fursa ya kufanya kazi kisheria kusambaza vifaa vya kijeshi, mafunzo kwa wafanyakazi katika vituo vya elimu na uhamasishaji wa teknlojia miongoni mwa wengine, ubalozi wa Nigeria umesema katika taarifa yake.
”Imeelezea makubaliano hayo kama maendeleo katika ushirikiano wa pande mbili baina ya Abuja na Moscow.