Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 23:51

Maelfu wajitokeza kupiga chanjo ya Covid 19 Afrika Magharibi

Nesi akimpiga mtu chanjo ya AstraZeneca ya COVID-19 kwa mwanamke mmoja katika hospitali ya taifa ya nchi hiyo mjini Abuja, Nigeria March 31, 2021.
Nesi akimpiga mtu chanjo ya AstraZeneca ya COVID-19 kwa mwanamke mmoja katika hospitali ya taifa ya nchi hiyo mjini Abuja, Nigeria March 31, 2021.

Kuibuka tena kwa visa vya virusi vya  corona huko Afrika Magharibi, makaburi yamefurika ambapo idadi ya mazishi inaongezeka na vitanda vya hospitali vimekuwa vichache.

Kuibuka tena kwa visa vya virusi vya corona huko Afrika Magharibi, makaburi yamefurika ambapo idadi ya mazishi inaongezeka na vitanda vya hospitali vimekuwa vichache.

Mabadiliko hayo yanayoonekana yanasukuma idadi kubwa ya watu waliokuwa wanasita kupiga chanjo wakati ambapo shehena ya chanjo kutoka kwenye vyanzo mbali mbali zinwasili baada ya kusimama kwa muda katika miezi ya karibuni.

Maelfu ya visa vipya vya COVID-19 vimeripotiwa katika eneo hilo katika wiki chache zilizopita huku kukiwa na viwango vya chini vya chanjo na kusambaa kwa virusi vipya vya delta, na nchi nyingine zinashuhudia idadi yao ni kubwa zaidi tangu janga hilo kuanza.

Wakazi ambao hapo awali walikuwa na wasiwasi wa kupiga chanjo wakati nadharia zisizo na uhakika zikienea mitandaoni sasa wamejitokeza kwa maelfu kutoka Liberia hadi Nigeria, Ghana na Senegal ili kupiga chanjo.

Mwanzoni, kulikuwa na watu ambao walitoa habari za uwongo, lakini wakati watu waligundua kuongezeka kwa vifo na habari za uongo, watu walielewa kuwa chanjo pekee ndiyo inaweza kuwaokoa, alisema Bamba Fall, Meya wa manispaa ya Medina katika mji mkuu wa Senegal, Dakar.

XS
SM
MD
LG