Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:29

Watu 20 watekwa na watatu kuuwawa Nigeria


Tangazo likionyesha kutafutwa kwa kiongozi wa kundi la boko haram Abubakar Shekau huko katuika kijiji cha Baga katika jimbo la kaskazini mashariki mwa jimbo la Bono. May 13,REUTERS.
Tangazo likionyesha kutafutwa kwa kiongozi wa kundi la boko haram Abubakar Shekau huko katuika kijiji cha Baga katika jimbo la kaskazini mashariki mwa jimbo la Bono. May 13,REUTERS.

Watu wenye silaha wamewaua watu watatu katika chuo cha kilimo katika jimbo la kaskazini magharibi mwa Nigeria la Zamfara na kuwateka nyara watu wengine 20

Watu wenye silaha wamewaua watu watatu katika chuo cha kilimo katika jimbo la kaskazini magharibi mwa Nigeria la Zamfara na kuwateka nyara watu wengine 20, wakiwemo wanafunzi 15, shule hiyo ilisema Jumatatu, katika tukio la utekaji nyara wa watu wengi.

Utekaji nyara wa kutumia silaha kwa ajili ya fidia sasa unagonga vichwa vya habari karibu kila siku katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika, miaka saba baada ya wenye msimamo mkali wa Boko Haram kushtua ulimwengu kwa kuchukua wasichana 276 kutoka Chibok.

Shule zinazolengwa na magenge ya wahalifu kaskazini na katikati mwa nchi hiyo kawaida huwa katika maeneo ya mbali ambapo wanafunzi hukaa katika mabweni na walinzi tu kwa usalama.

Siku ya Jumapili katika Chuo cha Kilimo na Sayansi ya Wanyama huko Bakura, watu wasiojulikana wenye silaha walishambulia shule hiyo saa 4 usiku msajili Aminu Khalid Maradun aliiambia AFP.

Walimuua polisi mmoja na maafisa wawili wa usalama, na kuwateka nyara watu 20, ikiwa ni pamoja na wanafunzi 15, alisema.

Wengine waliotekwa nyara ni wafanyakazi na wanafamilia. Afisa mwingine wa shule alithibitisha shambulio hilo.

XS
SM
MD
LG