Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 23:57

Watekaji nyara Nigeria wawaachilia watoto 28 kati ya 81


Wasichana waliotekwa nyara wa shule ya bweni katika jimbo la Zamfara baada ya kuachiwa huru Machi 2, 2021, Nigeria.
Wasichana waliotekwa nyara wa shule ya bweni katika jimbo la Zamfara baada ya kuachiwa huru Machi 2, 2021, Nigeria.

Watekaji nyara ambao walivamia shule ya bweni kaskazini mwa Nigeria mapema mwezi huu wamewaachilia watoto 28 Jumapili lakini wengine 81 bado wanashikiliwa, kulingana na mchungaji aliyehusika katika mazungumzo ya kuachiliwa kwao.

Shambulio la Shule ya Upili ya Bethel Baptist katika jimbo la Kaduna lilikuwa ni la kumi katika utekaji nyara katika shule tangu Desemba, kaskazini magharibi mwa Nigeria iliyofanywa na wanamgambo wa Kiislamu na hivi karibuni, magenge ya wahalifu.

Kundi la kwanza la watoto 28 liliachiliwa siku mbili baada ya uvamizi. Wazazi waliliambia shirika la habari la Reuters kwamba wanafunzi 180 kawaida Wanahudhuria shule hiyo, na kwamba wanafunzi walikuwa katika mchakato wa kufanya mitihani.

Wanafunzi ishirini na wanane wameachiliwa asubuhi ya leo, "Mchungaji Ite Joseph Hayab aliambia Reuters kwa njia ya simu ." Wanafunzi wengi kabla ya sasa walitoroka ... lakini 81 bado wako wamkamatwa.

"Polisi na kamishna wa jimbo la Kaduna wa usalama wa ndani na maswala ya nyumbani hawakupatikana mara moja kutoa maoni. Radika Bivan, mzazi ambaye binti yake ni miongoni mwa waliotekwa nyara alithibitisha kuwa 28 kati yao waliachiliwa lakini akasema hakuona mtoto wake kati yao.

Wanamgambo na magenge ya uhalifu wamesababisha taharuki nchini Nigeria ambapo wazazi wanadaiwa kuingia hofu kupeleka watoto wao shuleni.

XS
SM
MD
LG