Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 06:44

Jeshi la Nigeria lachunguza madai ya kuuawa kiongozi wa Boko Haram


 Abubakar Shekau
Abubakar Shekau

Msemaji wa jeshi la Nigeria Ijumaa amesema jeshi la nchi hiyo limeanzisha uchunguzi kuhusu madai ya kuuawa au kujeruhiwa vibaya kwa kiongozi wa kundi la Boko Haram, kufuatia mapigano kati ya kundi lake na wanamgambo wa Kiislamu.

Abubakar Shekau alianzisha uasi wenye itikadi kali ya Kiislamu mwaka 2009, na mashambulizi ya kundi lake la Boko Haram yaliuwa zaidi ya watu 30,000 na kulazimisha wengine millioni 2 kuhama makazi yako, pia kusababisha moja ya mizozo mibaya ya kibinadamu nchini Nigeria.

Ripoti nyingi zilizochapishwa Alhamisi kwenye vyombo vya habari vya Nigeria vikinukuu vyanzo vya ujasusi, zilisema Shekau alijeruhiwa au kuuwawa baada ya wapiganaji wake kupambana na wapiganaji wa kundi hasimu la Islamic State ambalo lilijitenga na Boko Haram tangu mwaka 2016.

Msemaji wa jeshi Mohammed Yerima amesema jeshi linafanya uchunguzi kuhusu madai hayo.

“Ni uzushi. Tunaufanyia uchunguzi. Tutatoa taarifa rasmi iwapo tutathibitisha madai hayo”, amesema msemaji huyo wa jeshi la Nigeria.

XS
SM
MD
LG