Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 11:12

Wanamgambo wenye itikadi kali wauwa wanajeshi watano Nigeria


Mwanajeshi wa Nigeria akifanya doria katika eneo la Polo, mjini Maiduguri, Nigeria ambalo mtu aliuawa February 16, 2019. REUTERS/Afolabi Sotunde
Mwanajeshi wa Nigeria akifanya doria katika eneo la Polo, mjini Maiduguri, Nigeria ambalo mtu aliuawa February 16, 2019. REUTERS/Afolabi Sotunde

Duru za kijeshi nchini Nigeria zinaeleza kuwa wanajeshi watano wameuawa pale wanamgambo waitikadi kali walipovamia ghafla msafara wao.

Wakati huohuo takriban raia 30 wametekwa nyara katika shambulio jingine.

Msafara wa wanajeshi ulioshambuliwa katika jimbo la kaskazini mashariki la Borno Jumamosi na wanamgambo ulishambulia pia msafara mwengine wa magari na kuwateka raia 35 katika jimbo hilo hilo siku moja kabla.

Shambulio la jana limetokea nje ya mji wa Mafa kaskazini wa mji mkuu wa jimbo hilo wa Maidiguri.

Afisa mmoja wa usalama anasema wanamgabo walifyatua gruneti kwa kutumia roketi na kuwauwa wanajeshi watano kwenye msafara huo.

Kundi la Boko Haram la Nigeria na kundi jingine lililojitenga la Iswap yamewauwa watu 36,000 na kualazimisha wengine milioni 2 kukimbia makazi yao mnamo muongo moja wa vita vyao dhidi ya serikali.

XS
SM
MD
LG