Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:26

Wimbi la pili la Virusi vya Corona laongezeka Afrika


Afrika kusini imeripoti maambukizi ya watu 10,000 kila siku kutokana na virusi vya Corona.

Waziri wa afya wa Afrika kusini amesema kwamba idadi ya maambukizi nchini humo imekuwa ikiongezeka kwa kiasi kikubwa, hasa katika Western cape, ikiwemo mji wenye shughuli za utalii wa Cape Town.

Nchini Nigeria, watu 930 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona jumatano, ikiwa ni idadi ya juu zaidi ya maambukizi kuwahi kurekodiwa kwa siku moja nchini humo.

Maambukizi mengi yameripotiwa katika mji mkuu wa kibiashara wa Lagos na katika mji wa Abuja.

Kufikia sasa, zaidi ya watu 75,000 wameambukizwa virusi vya Corona nchini Nigeria, 1,200 wamefariki.

Kuna wasiwasi kwamba nchi za Afrika zinakabiliwa na wimbi la pili la maambukizi ya virusi vya Corona, maambukizi yakiongezeka sana katika baadhi ya nchi zenye idadi kubwa ya watu tangu mwezi Septemba.

Afrika kusini imeripoti rasmi wimbi la pili la maambukizi, kwa kiasi cha zaidi ya asilimia 60 ya visa vinavyoripotiwa kila siku Afrika.

XS
SM
MD
LG