Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 03:36

Mlipuko wa kipindupindu Nigeria wauwa watu saba


Wafanyakazi wa afya wakitembelea jamii zilizoathiriwa na kipindupindu kutoa matibabu katika Jimbo la Adamawa, Nigeria. (Photo VOA Stringer Nigeria).
Wafanyakazi wa afya wakitembelea jamii zilizoathiriwa na kipindupindu kutoa matibabu katika Jimbo la Adamawa, Nigeria. (Photo VOA Stringer Nigeria).

Watu 7 wamekufa nchini Nigeria kutokana na mambukizi ya kipindupindu ambacho kimeathiri maeneo mengi nchini hasa katika majimbo ya kaskazini.

Kituo cha kudhibiti magonjwa Nigeria NCDC kinasema ni muhimu sana kuhamasisha usafi wa mazingira na kila mtu kufuata kanuni za kujikinga za ugonjwa na kutumia maji kutoka kwenye vyanzo safi tu kama hatua ya kwanza ya kuambana na kusambaa kwa kipindupindu.

Tukio hili liliripotiwa kwa mara ya kwanza mwezi wa Januari katika jimbo la Bauchi ambalo lina idadi kubwa ya wagonjwa takribani watu 1,239 kati ujumla ya 14,393 kote nchini.

Katika uchambuzi wake juu ya sababu ya ugonjwa huu kutokea, Rais wa Umoja wa Madaktari wa Nigeria Dkt Innocent Ujah anasema ni bahati mbaya kwamba Wanigeria bado wanakufa kutokana na ugonjwa kama kipindupindu katika karne ya 21.

Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Nigeria kinasema kati ya January na Juni mwaka huu jumla ya watu 14,393 wameambukizwa kipindipindu katika majimbo 15 pamoja na mji mkuu Abuja. Watu 325 wamekufa wakiwemo watu 7 ambao walikufa mjini Abuja. Mtaalamu wa masuala ya Afya ya Umma Dkt. Abiodun Paul anasema hii ni hasara kubwa.

Dkt Laz Eze mtaalam wa afya ya umma anasema mfumo wa huduma za Afya za msingi kwa jamii unapaswa kuimarishwa hasa katika utoaji elimu kwa umma ili kipindupindu kiweze kuiziliwa kwqsababu ugonjwa huo unaweza kuua mtu yeyote ikiwa haukushughulikiwi vzuri.

Mfamasia ambaye mwanawe alikumbwa na kipindupindu, Musa Aliyu ana sema watu hawa paswi kutegemea maji kutoka vyanzo visivyokuwa na uhakika kwasababu hiyo ni moja wapo ya chanzo cha kipindupindu.

Katika data ya maambukizi baina ya June na sasa, watu saba wamekufa kutoka ujumla ya watu 91 walio athiriwa katika wilaya ya Abuja mji mkuu wa Nigeria. Katika majimbo 6 kaskazini mwa Nigeria asilimia 51 ya wathirika ni wanaume. Maambukizi ya Kipindipindu hutokea wakati wa msimu wa mvua nchini Nigeria. Serekali ime anza kutoa elimu kwa umma katika maeneo ya vijijini.

Kutoka Lagos jina langu ni Collin Atohengbe kwa idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika, Washington.

XS
SM
MD
LG