Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 06:48

Bilionea Mwafrika Aliko Dangote kuuza mbolea Marekani


Aliko Dangote
Aliko Dangote

Kiwanda cha mbolea cha billiyonea wa Nigeria Aliko Ndangote ambacho kiko karibu na mji wa Lagos kitasafirisha shehena yake ya kwanza kwenye jimbo la Marekani la Lousiana mwishoni mwa mwezi huu wa Juni au mapema mwezi Julai, huku mbolea nyingi ikitarajiwa kupelekwa Brazil, Dangote amesema.

Kiwanda hicho kipya, ambacho kina uwezo wa kutengeneza tani millioni 3 za mbolea ya Urea kwa mwaka, kitakua na uwezo wa kusambaza mbolea kwenye masoko makuu ya kusini mwa jangwa la Sahara, Dangote aliuambia mkutano wa uchumi kwa njia ya mtandao ulioandaliwa na Qatar.

Dangote amesema “mbali na kukidhi mahitaji ya ndani, tutaweza kupata pesa nyingi kwa kusafirisha bidhaa zetu kwenda nchi za Amerika kusini”.

XS
SM
MD
LG