Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 18:21

Wezi wa ng'ombe wauwa 35 na kuchoma nyumba moto Nigeria

Watu wakiandamana katika mitaa ya Kaduna kulaani utekaji nyara mwengine wa watu 16, katika eneo la halmashauri la Kaduna, Nigeria, Julai 8, 2021. (Foto: REUTERS/Bosan Yakusak)
Watu wakiandamana katika mitaa ya Kaduna kulaani utekaji nyara mwengine wa watu 16, katika eneo la halmashauri la Kaduna, Nigeria, Julai 8, 2021. (Foto: REUTERS/Bosan Yakusak)

Polisi nchini Nigeria wamesema Jumamosi wezi wa ng'ombe waliyokuwa na silaha wamewaua karibu watu 35 katika vijiji vitano jimbo la Zamfara kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Mauaji hayo yametokea katika jimbo linaloendelea kukumbwa na ghasia na utekaji nyara wa watu.

Hata hivyo wanavijiji wanasema watu 43 ndiyo waliyouawa kwenye shambulio lililotokea siku ya Alhamisi usiku.

Msemaji wa polisi wa jimbo hilo Mohammed Shehu ameliambia shirika la habari la AFP kwamba majambazi hao wakiwa kwenye pikipiki walifanya mashambulio katika vijiji vya mbali na kutia nyumba za wakazi moto katika wilaya ya Maradun.

Amesema wahuni hao walifanikiwa kukimbia kabla ya maafisa wa usalama kuwasili katika Eneo hilo lisilo na barabara nzuri.

Maeneo yanayopitia vitendo vya utekaji nyara na mauaji katika jimbo la Kaduna Nigeria.
Maeneo yanayopitia vitendo vya utekaji nyara na mauaji katika jimbo la Kaduna Nigeria.

Maeneo ya kaskazini magharibi na kati ya Nigeria yamekuwa yakishambuliwa hivi karibuni na magenge ya wezi wa ngombe na watekaji nyara wanaoshambulia vijiji, kuwauwa watu na kuwateka wakazi kwa ajili ya kudai fidia pamoja na kuiba mifungo na kutia moto nyumba za wakazi.

Chanzo cha Habari : AFP

XS
SM
MD
LG