Uamuzi huo ulifikiwa baada ya kampuni hiyo kubwa ya Marekani kufuta ujumbe wa tweet kutoka akaunti ya rais Muhammadu Buhari, wakidai kuwa ulikukiuka kanuni zake.
Mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu pia yamelaani hatua hiyo, ambayo ilifuatia majaribio ya hapo awali ya serikali ya nchi yenye watu wengi zaidi barani Afrika, kudhibiti mitandao ya kijamii.
Makampuni ya simu ya Nigeria yalitii agizo la serikali Ijumaa, kusitisha huduma za Twitter kwa muda usiojulikana.
Ujumbe wa kidiplomasia wa EU, Marekani ,Uingereza, Canada na Ireland, umetoa taarifa ya pamoja leo Jumapili kulaani hatua hiyo.
"Kupiga marufuku mifumo ya kujieleza sio jibu," ilisema taarifa hiyo. Zaidi ya Wanigeria milioni 39 wana akaunti za Twitter, kwa mujibu wa taasisi za utafiti.