Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 22:43

Mkuu wa jeshi na maafisa 10 wafariki katika ajali ya ndege Nigeria


Maafisa wa jeshi wakiwa wamebeba jeneza la hayati mkuu wa jeshi la Nigeria Ibrahim Attahiru aliyefariki katika ajali ya ndege Ijumaa.
Maafisa wa jeshi wakiwa wamebeba jeneza la hayati mkuu wa jeshi la Nigeria Ibrahim Attahiru aliyefariki katika ajali ya ndege Ijumaa.

Nigeria imegubikwa katika huzuni kubwa kufuatia kifo cha mkuu wa jeshi na maafisa wengine 10 katika ajali ya ndege iliyo tokea katika uwanja wa ndege wa Kaduna mwishoni mwa wiki.

Ripoti za awali zimebaini kuwa upepo mkali ulisababisha ajali hiyo wakati ndege ilipokuwa inatua. Uchunguzi zaidi unaendelea kuhusu ajali hiyo.

Mkuu wa jeshi la Nigeria Ibrahim Attahiru alikuwa safarini kuhudhuria sherehe ya mahafali ya maafisa wapya wa Jeshi wa Chuo cha Ulinzi mjini kaduna, kaskazini mwa Nigeira.

Afisa wa idara ya anga katika Uwanja Ndege wa Kaduna, Amina Salami amesema ndege hiyo ambayo ilikuwa imembeba Lt. Gen. Ibrahim Attahiru na Maafisa wengine 10 ilipangwa kutua katika kituo cha Jeshi lakini kwasababu ya hali ya hewa ndege ilielekezwa kwenda kutua katika uwanja wa ndege wa kiraia ambako ilipata ajali hiyo.

Katika hafla ya mazishi ya maafisa hao 11 mjini Abuja, Mkuu wa Majeshi wa Ulinzi Jenerali Lucky Irhabor amesema maafisa hao wote waliopoteza maisha yao katika huduma kwa taifa lakini watabakia kuendelea na vita vya kuhakikisha usalama wa nchi.

Katika ujumbe wake kupitia kwa Waziri wa Ulinzi Ibrahim Magagshi Rais Mohammadu Buhari alisema Nigeria imepoteza maafisa wa jeshi ambao walikuwa wakishughulikia suala la umoja wa Nigeria.

Luteni Jenerali Attahiru alikuwa mtu mwenye bidii ya juu ambaye alitumia muda wake kazini kuonyesha bidii yake katika kazi kutekeleza wajibu katika kufanikisha kazi zake, ikiwa ni juhudi za kulipunguzia nguvu kundi la boko haram.

Tangu kuteuliwa kwake tarehe 4 mwezi wa Marchi mwaka huu, ameongoza jeshi kwenye vita vingi na kushinda dhidi ya majambazi na vikundi vya kigaidi kaskazini mashariki mwa Nigeria. Kifo cha luteni Jenerali Ibrahim Attahiru ni msiba mkubwa kwa familia yake ambao wamemuelezea kama baba mzuri sana, Jeshi la Nigeria na Wanigeria kwa ujumla.

Na mwandishi wetu Collins Atohengbe-Lagos.

XS
SM
MD
LG