Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:24

Nigeria yapokea dozi milioni 4 za chanjo ya Moderna kutoka Marekani


Rais wa Nigeria Muhamamadu Buhari akionyesha cheti cha chanjo ya corona.
Rais wa Nigeria Muhamamadu Buhari akionyesha cheti cha chanjo ya corona.

Nigeria imepokea dozi milioni 4 za chanjo ya Moderna dhidi ya  COVID-19 iliyotolewa na serikali ya Marekani.

Nigeria imepokea dozi milioni 4 za chanjo ya Moderna dhidi ya COVID-19 iliyotolewa na serikali ya Marekani, waziri wa afya wa Nigeria alisema Jumatatu, wakati nchi hiyo ya Afrika Magharibi ikipambana na wimbi la tatu la maambukizo.

Osagie Ehanire alisema chanjo hizo, ambazo zilifika Jumapili, zinaendelea kuthibitishwa na mdhibiti wa dawa nchini humo. Alisema dozi hizo zitasambazwa kwenye majimbo ya eneo hilo mara tu zitakapothibitishwa kuwa zinafaa kutumiwa.

Serikali ya Marika wiki iliyopita ilisafirisha karibu dozi milioni 10 kwa nchi mbili za Afrika zenye idadi kubwa ya watu - Nigeria na Afrika Kusini.

Chanjo nchini Nigeria inapaswa kuanza hivi karibuni na kuwasili .kwa chanjo ya Moderna, shukrani kwa serikali ya Marekani, Ehanire aliuambia mkutano kuhusu corona huko Abuja.

Alisema Nigeria ingeweza kupokea dozi zaidi ya milioni 40 ifikapo mwishoni mwa mwaka, bila kutoa maelezo zaidi.

XS
SM
MD
LG