Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:37

Ajali eneo la ujenzi Nairobi laua nane, watu wawili wajeruhiwa


Ramani ya Kenya
Ramani ya Kenya

Watu nane, ikiwa ni pamoja na Wachina wawili, walikufa na wengine wawili wamejeruhiwa Alhamisi baada ya kreni kuanguka katika eneo la ujenzi katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, polisi wamesema.

Kreni hiyo ilianguka wakati wa kazi ya kujenga hosteli ya wanafunzi ya ghorofa 14.

Tumepoteza watu wanane, alisema Andrew Mbogo, mkuu wa polisi wa kitongoji cha Kilimani, ambapo ajali ilitokea.

Ni pamoja na Wachina wawili na Wakenya sita, aliwaambia waandishi wa habari.

Chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika mara moja lakini mashuhuda wa tukio hilo walisema walisikia watu wakipiga kelele wakati kreni ikianguka chini.

Tulikuwa tukila chakula cha mchana wakati tulisikia vitu vikianguka na tukidhani sehemu ya jengo hilo ilikuwa ikishuka, mfanyakazi wa ujenzi Michael Odhiambo aliiambia AFP.

Tulipofika huko, tuligundua kuwa kreni ilikuwa imeanguka chini, akaongeza.

Ujenzi mbovu na kukiukwa kwa kanuni kumesababisha ajali nyingi mbaya huko Nairobi.

Kenya inapitia kipindi cha ongezeko la ujenzi lakini ufisadi umeruhusu wakandarasi kupita njia za pembeni au kuzikwepa kanuni.

XS
SM
MD
LG