Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:59

Kenya: Mahakama ya rufaa yatupilia mbali marekebisho ya Katiba maarufu BBI


Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa upinzani Raila Odinga,. (Facebook/Uhuru Kenyatta)
Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa upinzani Raila Odinga,. (Facebook/Uhuru Kenyatta)

Mahakama ya Rufaa ya Kenya Ijumaa imetupilia mbali hatua ya serikali kufanya marekebisho ya msingi katika Katiba, maarufu kama BBI, ikiwa ni pigo jipya kwa Rais Uhuru Kenyatta ambaye alianzisha mapendekezo hayo yenye utata.

Jopo la majaji saba limekubaliana na uamuzi wa awali wa Mahakama Kuu kwamba namna ambavyo mabadiliko yalianzishwa yalikuwa kinyume cha sheria, uamuzi ambao utabadilisha mwelekeo wa kisiasa ikiwa umebakia chini ya mwaka mmoja kabla ya uchaguzi kufanyika nchini.

Rais Kenyatta alitetea akidai kuwa hatua hiyo itazifanya siasa kuwa shirikishi zaidi na kusaidia kumaliza mzunguko wa ghasia za uchaguzi nchini, jambo ambalo limewagawanya wanasiasa.

Rais wa Mahakama Daniel Musinga alitoa uamuzi kuhusu rufaa ya serikali juu ya uamuzi uliokuwa umetolewa awali baada ya zaidi ya saa 10 ya kauli za majaji zilizorushwa moja kwa moja katika televisheni na vyombo vingine vya habari.

“Rais hana mamlaka chini ya Katiba kufanya mabadiliko yoyote katika katiba,” alisema Musinga.

“Mabadiliko ya katiba yanaweza tu kuanzishwa na bunge… au kwa uanzilishi wa waliowengi,” aliongeza na kuongaza kuwa Kenyatta anaweza kushtakiwa katika mahakama ya madai kwa kuanzisha mchakato huo.

Walioshindwa katika kesi hiyo wana uhuru wa kukata rufaa kwenye mahakama kuu, ambayo ndiyo ya mwisho katika mfumo wa mahakama wa taifa hilo la Afrika Mashariki.

Hata hivyo, muda mfupi baada ya uamuzi huo, kiongozi wa upinzani nchini humo, Raila Odinga, aliandika ujumbe kupitia mtandao wa Twitter na kusema kuwa mahakama ya rufaa ilikuwa imetekeleza jukumu muhimu, na kuongeza, "sisi tunaonelea ni wakati wa kusonga mbele."

XS
SM
MD
LG