Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:10

Matukio makuu Afrika mwaka 2020


Uvamizi wa nzige

Nchi kadhaa za Afrika mashariki hasa Kenya, Uganda, Sudan kusini, Somalia, Ethiopia na sehemu za jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, zilishuhudia wimbi kubwa la nzige ambalo lilisababisha uharibifu mkubwa kwa mime ana kutishia kutokea baa la njaa, mwanzoni mwa mwaka 2020.

Nzige hao wa jangwani walivamia mataifa ya Afrika mashariki kwa kiwango ambacho kilisababisha wasiwasi mkubwa kati ya rai ana serikali kuhusu uwezekano wa ukosefu wa chakula kutokana uharibifu mkubwa kwa mimea.

Uvamizi wa nzige hao ulitajwa kuwa mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika mda wa miaka 60. Walijaa shambani, msituni, barabarani na popote palipokwa na majani.

Serikali zilitumia ndege kunyunyuzia dawa wadudu hao bila mafanikio. Waliendelea kuzaana kwa kasi na kusababisha uharibifu mkubwa shambani.

Shirika la chakula ulimwenguni FAO, lilitoa ombi la kimataifa, la msaada wa dola milioni 76 kwa ajili ya kukabiliana na nzige hao. Dola milioni 33 zilipatikana, huku umoja wa mataifa ukitoa wito wa msaada zaidi.

Mgogoro wa kisiasa DRC

Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo hali ya kisiasa mwaka huu 2020 imekuwa ya msukosuko, licha yam waka kuanza kwa utulivu baada ya kuapishwa kwa rais Felix Tshisekedi. Mwaka unapokamilika, ushirikiano kati ya rais Tshisekedi na mtangulizi wake Joseph Kabila unaendelea kuyumba yumba.

Hakuna mengi yaliyobadilika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo mwaka 2020 ikilinganishwa na mianka mingine kando na mabadiliko ya rais.

Baada ya Joseph Kabila kuondoka madarakani na kumpokeza Felix Tshisekedi katika hatua ya kihistoria ya ubadilishanaji madaraka kutoka utawala mmoja hadi mwingine, mgogoro wa madaraka bado unaendele anchini humo.

Muungano wa vyama vinavyomuunga mkono rais mstaafu Joseph Kabila – FCC, umeendelea kugawanyika baada ya wabunge kumpindua spika wa bunge kutoka chama chake Kabila, Jeanine Mabunda.

viongozi wa FCC wamelaumiwa kwa upendeleo na ubaguzi na hivyo kuangusha muungano kati ya Kabila na Tshisekedi.

Mashambulizi ya waasi DRC

Mashambulizi kutoka kwa makundi ya wapiganaji ya maimai, Allied democratic forces ADF, Lords resistance movement LRA miongoni mwa makundi mengine, yameendelea kusababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali licha ya rais Tshisekedi kuanzisha msako mkali dhidi ya wapiganaji hao hasa sehemu za mji wa Beni.

Umoja wa mataifa umeeleza wasiwasi kuhusu hali ya usalama saw ana mzozo wa siasa usiomalizika. Umoja huo umeonya kwamba mzozo huo unaweza kudhoofisha nchi hiyo na kurudisha nyumba madanikio yaliyopatikana.

Burundi: Nkurunziza afariki, Ndayishimiye aingia madarakani

Mwezi Juni Burundi iliomboleza kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza, siku chache kabla ya kumpokeza madaraka Evariste Ndayishimiye. Kifo cha Nkurunziza kilighubika uvumi mwingi, serikali ikikanusha kwamba alikuwa amekufa kutokana na virusi vya Corona.

Nkurunziza aliaga dunia Juni 9, akiwa na umri wa miaka 55. Serikali ilisema kwamba alifariki kutokana na mshutuko wa moyo.

Mke wake alikuwa amelazwa katika hospitali moja Nairobi Kenya, katika kile kiliripotiwa kama maambukizi ya virusi vya Corona.

Kifo chake kilikatika ghafla sherehe ya ushindi wa Evariste Ndayishimiye kuongoza taifa hilo kutoka kwa Nkurunziza aliyekuwa anamalizia mda wake madarakani. Ndayishimiwe ambaye alikuwa amependekezwa na Nkurunziza kugombea urais, aliapishwa na kuingia madarakani.

Tume huru ya uchaguzi nchini Burundi CENI, ilimtangaza jenerali Evariste Ndayishimiye wa chama cha CNDD-FDD kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi May, baada ya kupata asilimia 69 ya kura.

Upinzani ukiongozwa na Agathon Rwasa hata hivyo ulidai kuwepo udanganyifu mkubwa katika hesabu ya kura.

Mapnduzi ya kijeshi Mali

Jeshi la Mali lilimuondoa madarakani Rais Ibrahim Boubacar Keita mwezi Agosti. Hali ya mgogoro hata hivyo inaendelea nchini humo licha ya kuwepo serikali ya mpito na juhudi za kutaka kuandaa uchaguzi mpya.

Mapinduzi hayo yaliongozwa na mkuu wa majeshi Kanali Assimi Goita, mwenye nguvu nchini Mali, na kuamuru rais Boubakar keita kujiuzulu na kutengua bunge na serikali.

Mapinduzi yalikemewa na viongozi katika kanda ya Sahel, umoja wa Afrika, umoja wa ulaya na umoja wa mataifa, wakitaka kurejeshwa kwa utawala wa kiraia.

Viongozi wa mapinduzi hayo walisema sababu kuu ilikuw akurejesha utulivu nchini humo kufuatia maandamano ya kupinga mashambulizi ya makundi ya waasi.

Mali imekumbwa na mashambulizi kutoka kwa makundi ya wapiganaji kila mwaka, ambayo yamesababisha vifo, majeruhi na watu kukoseshwa makao.

Misukosuko ya kisiasa pia ilishuhudiw akatika nchi za Niger, Burkinafaso, Chad na Mauritania ambako pia kuna makundi ya wapiganaji yanayotekeleza mashambulizi kila mara.

Maandamano Nigeria

Nchini Nigeria zaidi ya watu 70 waliuawa kutika maandamano dhidi ya ukatili wa polisi.

Maandamano hayo yalianza tarehe 7 mwezi Oktoba vijana wakidai kuvunjwa kwa kikosi cha polisi cha SARS walichokishutumu kwa mauaji ya kiholela na kuvunja haki za kibinadamu.

Kikosi hicho kilivunjwa baadae, lakini maandamano yaliendelea n ahata kushika kasi baada ya mashambulizi ambayo Amnesty International lilisema kuwa vikosi vya usalama viliua watu karibu 12 kwa kuwapiga risasi.

Rais Muhammadu Buhari alisema kwamba waliopoteza maisha ni raia 51, polisi 11 na wanajeshi saba, katika maandamano hayo mabaya zaidi kuwahi kutokea Nigeria katika siku za hivi karibuni.

Sudan yaondolewa kwenye orodha ya wafadhili wa Ugaidi duniani

Marekani iliiondoa Sudan katika orodha ya wafadhili wa ugaidi duniani baada ya kulipa fidia yad ola milioni 335 kwa waathiriwa na familia ya shambulio la bomu lililotekelezwa na kundi la al-Qaeda mwaka 1998 dhidi ya ubalozi wa marekani mjini Nairobi Kenya na Dar-es-salaam Tanzania.

Sudan iliorodheshwa mwaka1993 wakati kiongozi wa al-Qaeda Osama Bin Laden alipoishi nchini humo kama mgeni wa serikali.

Sudan pia ilikubali kuimarisha uhusiano wake na Israel chini ya makubaliano yaliyosimamiwa na rais wa Marekani Donald Trump.

Nchini Ivory coast, Allasane Outtara alipata ushindi wa kishindo, wa asilimia 94.3 ya kura katika uchaguzi mkuu na kusalia madarakani kwa mhula wa tatu baada ya kubadilisha katiba ya nchi hiyo kumrushu kugombea mhula mwingine madarakani.

Uchaguzi huo ulikumbwa na machafuko ya kabla ya uchaguzi. Karibu watu 30 waliuawa katika machafuko hayo.

Rwanda: Rusesabagina akamatwa

Nchini Rwanda mkosoaji wa Serikali ya rais Paul Kagame Paul Rusesabagina, alikamatwa na kurudishwa Rwanda ambako alifunguliwa mashataka kadhaa yakiwemo kupanga kupindua serikali ya Kagame.

Hali ya sintofahamu bado inazunguka namna Rusesabagina alivyokamatwa.

Rusesabagina anatuhumiwa kwa kuunda na kuongoza chama cha kigaidi pamoja na mtandao wa vyama vya kigaidi ikiwemo MRCD na PDR-Ihumure kwa lengo la kutekeleza mapinduzi nchini Rwanda.

Siasa za BBI zatawala mwaka 2020 Kenya

Siasa za kuunda jopo la maridhiano maarufu kama BBI zimetawala mwaka mzima nchini Kenya. Japo nia ya BBI ni kuunganisha nchi, mchakato huo umebuni makundi mawili nchini humo, kundi moja likiongozwa na naibu war ais William Ruto na lingine likiongozwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga Pamoja na rais Uhuru Kenyatta.

Tanzania: Magufuli ashinda mhula wa pili

Nchini Tanzania rais John Pombe Magufuli alishinda mhula wa pili madarakani kwa kupata ushindi mkubwa uliopingwa na upinzani kutokana na tuhuma kubwa za udanganyifu.

Mahufuli alipata asilimia 84 ya kura zilizopigwa na kumshinda mpinzani wake mkuu Tundu Lissu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kwa zaidi ya kura milioni kumi. Lissu alipata kura milioni 1.9.

Chama chake Magufuli kilishinda viti vingi vikiwemo vya bunge. Mgawanyiko ulionekana ndani ya chama kikuu cha upinzani CHADEM, baada ya baadhi ya wanachama wake kuapishwa katika viti maalum, wakati baadhi ya viongozi wa chama walisema hawakujua aliyewateua.

Wanasiasa kadhaa wa upinzani walidai kutishiwa maisha, akiwemo Tundu Lisu aliyetorokea Ubelgiji huku aliyekuwa mbunge Gdbless Lema akikimbilia Canada.

Mapigano Tigray, Ethiopia

Nchini Ethiopia mapigano mabaya yalitokea katika eneo la Tigray, jeshila Ethiopia likishambulia vikosi vya Tigray.

Hii ni baada ya waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kuamrisha mashambulizi dhidi ya vikosi vya Tigray baada ya kuripotiwa kushambulia kambi ya jeshi la Ethiopia mjini Mekelle.

Idadi ya watu wasiojulikana walifariki dunia na maelfu ya raia wa Ethiopia kukimbilia Sudan kama wakimbizi.

Museveni agombea mhula wa 6 madarakani, hana mpango wa kustaafu

Na nchini Uganda joto la kisiasa linaendelea kuongezeka wakati tunakamilisha mwaka.

Rais Yoweri Museveni ambaye amesema hana nia ya kuondoka madarakani, anagombea mhula wa sita.

Museveni anakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa wagombea wengine 10 akaiwemo mwanamuziku Rober Kyagulanyi, maarufu Bobi wine.

Uchaguzi wa Uganda utafanyika Januari 14 2021.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG