Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:43

Kenyatta atangaza mikakati mitatu ya serikali yake


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema serikali itakuwa na jukumu kuu kuanzia mikakati ya kuwakinga raia wake dhidi ya janga la virusi vya corona, kuwekeza kwa vijana na kutatua tatizo sugu la umiliki wa ardhi.

Rais Kenyatta alisema hayo katika hotuba yake kwa bunge la nchi hiyo ambapo ameelezea hali hali ya nchi na mkakati wa serikali katika kukabiliana na janga la Covid 19 katika taifa hilo.

Amesema kuwa serikali yake pia itaendelea kuwekeza kwa vijana, ili kuwapa uwezo wa kujikimu kimaisha na kuchangia katika maendeleo ya taifa la Kenya.

Pia ameelezea kuwa hatua madhubuti zitachukuliwa ili kutatua tatizo sugu la umiliki wa ardhi nchini Kenya, ambapo serikali yake imetoa hatimiliki takriban milioni 5 kwa kipindi cha miaka saba.

Kwa mujibu wa katiba ya Kenya kipengele cha 132 na kanuni za kudumu za bunge zinampa Rais Kenyatta fursa ya kulihutubia bunge kila baada ya mwaka mmoja kuelezea mafanikio ya serikali, miradi iliyopo na uwezo wa kuwasaidia raia wake, hali ya usalama wa nchi, mahusiano na mataifa ya kigeni na muongozo wa utekelezaji wa katiba na mikataba ya kimataifa.

Rais p[ia katika hotuba yake ameelezea kuwa nchi inajikuta katika mazingira mapya ya maambukizi ya virusi vya corona ambavyo mpaka hivi sasa vimesababisha vifo vya watu 1,203 na wengine 66,723 wakipata maambukizi.

Hata serikali yake inaendelea kujikuta katika kile kinachoelezewa wimbi jipya la maambukizi ya virusi vya corona. Rais Kenyatta amesema seriakli yake inajivunia wahudumu wake wa afya wanaendelea kujitolea kuikinga nchi dhidi ya makali ya virusi hivyo.

“Tunajivunia wahudumu wetu wa afya na tutaendelea kujivunia juhudi zzao katika mazingira haya magumu,” amesema Rais.

Rais amesisitiza kuwa bunge linahitaji kupitisha sheria itakayoongoza kuitishwa kwa kura ya maoni ili kuiwezeshga nchi kufanikisha mchakato wa kufanyia marekebisho katiba ya nchi, kupitia jopo la maridhiano liitwalo BBI.

Kenyatta amesema kuwa ataendelea kusimamia juhudi za kuleta amai, umoja na kujumuisha wote katika serikali, na kwamba taifa huenda halipata nafasi nyingine kufanya mabadiliko hayo muhimu katika sheria zake.

Katika hotuba yake Rais pia ametoa maelekezo kwa waziri wa elimu, Prof. George Magoha katika muda wa siku 14 kutangaza kalenda mpya ya masomo kwa mwaka 2021. Serikali pia imetangaza kuwa inajenga madarasa mapya 12,500 na vituo vingine vya masomo na mfumo mpya wa ujenzi wa vituo vya masomo kutolea kabla ya mwezi Desemba.

Mwishowe, Kenyatta amzindua kanuni za kudumu za bunge la taifa kwa lugh ya Kiswahili, ikimaanisha kuwa bunge hilo litakuwa linafaya mijadala yake kwa lugha ya Kiswahili kila Alhamisi, kila wiki.

-Imetayarishwa na Kennedy Wandera, VOA, Nairobi.

XS
SM
MD
LG