Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:44

Serikali ya Kenya yasema bima ya NHIF haiwezi kutumika kugharamia matibabu ya Corona


Serikali ya Kenya imesema kwamba haiwezi kugharamia matibabu kwa wagonjwa wa Corona nchini humo kupitia bima ya afyaya NHIF kwa sababu matibabu hayo ni ghali sana.

Raia wa Kenya mwenye bima ya NHIF hulipia kila mwezi mfuko huo ili kugharamia matibabu mbalimbali yakiwemo ya dharura.

Hatua hiyo inajiri wakati Kenya inapambana na wimbi la pili la maambukizi ya virusi vya Corona, idadi ya watu wanaoambukizwa ikiendelea kuongezeka kila siku.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe ameambia kamati ya bunge ya afya jumatano kwamba matibabu ya corona ni ghali sana kwamba serikali haiwezi kumudu kugharamikia katika hospitali za umma au za kibinafsi.

“Tuna bahati kuwa visa vingi tulivyonavyo vinahusu watu walio na mifumo ya bima ya afya ya kibinafsi, na kampuni hizo zinawafaidi. Lakini linapokuwa suala la magonjwa ya kawaida, serikali kupitia NHIF itatekeleza wajibu wake. Kisha serikali inaweza kuongeza mfuko huo.” Amesema Kagwe.

Kwa kawaida, serikali hulipia ada hizi kwa wote waliojiunga na wanalipia kila mwezi kuwawezeisha mwananchi kufikia huduma maalum za matibabu kote nchini katika hospitali za umma na za kibinafsi.

NHIF pia hugharamia mahitaji ya matibabu ya ghafla na huwa nafuu kwa wagonjwa wenye kipato cha chini.

Serikli ya Kneya imesema kuwa kila mkenya atakayeugua corona, atagharamia matibabu yake.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema kwamba kwa kawaida, serikali huwa haigharamii matibabu kutokana na magonjwa kama janga la corona kwa sababu utakuwa mzigo mkubwa kwa serikali.

Kwa sasa, inagharimu dola 100 kupima virusi vya Corona, kila mtu. Gharama hiyo imepelekea wakenya wengi kukosa kujipima na kutambua iwapo wameambukizwa virusi hivyo.

Wakenya wameishutumu serikali kutokana nah atua hiyo. Wameikashifu serikali kupitia kwa mitandao ya kijamii wakisema haijali kabisa raia wake wanaofanya kazi kwa bidii kila siku kujenga uchumi wa nchi hiyo.

Idadi ya watu mabao wanathibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona sawa na vifo, inaendelea kuongezeka kila siku nchini Kenya.

Imetayarishwa na mwandishi wetu wa Nairobi Kennedy Wandera

XS
SM
MD
LG