Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 18:05

Wakili kutoka Kenya ajisalimisha ICC kujibu madai ya kuhonga mashahidi


Naibu wa rais wa Kenya William Ruto (kulia)
Naibu wa rais wa Kenya William Ruto (kulia)

Wakili mmoja wa Kenya amejisalimisha kwa viongozi wa Uholanzi ili kukabiliana na mashtaka dhidi yake kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC).

Wakili huyo anadaiwa kuwahonga mashahidi katika kesi dhidi makamu rais wa Kenya William Ruto katika mahakama hiyo.

Wakili Paul Gicheru alikuwa anatafutwa na warranti ya ICC tangu mwaka wa 2015, akishtumiwa kujaribu kuwapa hongo mashahidi 6 wa muendesha mashtaka ili wabadili Ushahidi wao katika kesi dhidi ya William Ruto.

Ruto na mwanahabari Joshua Sang, walishtakiwa kwa kuchochea ghasia za kikabila baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata wa mwaka 2007 ambapo watu elfu 1,200 waliuwawa.

Mwaka 2016, majaji waliamuru kwamba hakuna kesi yoyote ya kufuatilia, licha ya kuwa walitoa nafasi ya kupokea mashtaka mapya, wakihisi kwamba kesi hiyo ilidhoofishwa na muingilio wa siasa na vitisho dhidi ya mashahidi.

Kulingana na shirika la habari la Reuters, msemaji wa Ruto hakupendelea kutoa maelezo yoyote kuhusu kesi ya wakili Gicheru, lakini amesisitiza kwamba Gicheru hakuwahi kufanya kazi kama wakili wa Ruto.

Reuters haikufanikiwa kumpata muakilishi wa Gicheru.

Katika taarifa, ICC iliwaomba viongozi wa Uholanzi kumfikisha mahakamani Gicheru, mara tu utaratibu wa kumkamata utakapomalizika.

Kesi nyingine inayodai kuhusika kwa rais Uhuru Kenyatta katika ghasia baada a uchaguzi wa mwaka 2007 ilitupiliwa mbali na mahakama hiyo mwaka 2015.

Imetayarishwa na Patrick Nduwimana, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG