Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:57

Maambukizi ya Corona yaongezeka kwa kasi Kenya, masharti yarejeshwa


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

Serikali ya Kenya imetangaza kurejesha baadhi ya masharti yaliyokuwa yametolewa awali katika kupambana na wimbi jipya la maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo.

Rais Uhuru Kenyatta amesema kwamba kila dalili zinaonyesha kuwa wimbi jipya la maambukizi ya virusi vya Corona linasambaa nchini humo.

Ameamuru kuongeza muda wa watu kusalia nyumbani saa za usiku na pia akapiga marufuku mikutano yote ya siasa.

Wizara ya afya ya Kenya imesema kwamba inamulika hali ya maambukizi nchini humo kwa mda wa wiki mbili jizajo, kabla ya kutanhaza masharti zaidi iwapo itahitajika kufanya hivyo.

Maambukizi ya virusi vya Corona yameongezeka kwa asilimia 16 mwezi Oktoba, mwezi mmoja baada ya Kenya kulegeza baadhi ya masharti yaliyokuwa yameekwa kudhibithi maambukizi.

Kuongezeka kwa maambukizi

Kabla ya kulegeza masharti hayo, kiwango cha maambukizi kilikuwa kimeshuka na kufikia asilimia 4, maana kwamba yameongezeka mara nne katika kipindi cha siku thelathini.

Watu 15,000 wameambukizwa virusi hivyo na 300 kufariki katika kipindi cha mwezi mmoja.

Serikali inasema kwamba maambukizi yameongezeka kutokana na tabia ya wakenya kupuuza kutilia maanani namna ya kujiepusha na maambukizi na kukomesa kusambaa kwa virusi hivyo.

Hata hivyo, wanasiasa wakuu nchini Kenya wakiongozwa na rais Uhuru Kenyatta, naibu wake William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga wamekuwa wakiandaa mikutano mingi ya hadhara, yenye idadi kubwa ya watu, na bila ya kuzingatia maagizo ya afya ya kuzuia virusi vya Corona kusambaa.

Masharti ya Kenyatta

Kenyatta sasa amepiga marufuku mikutano hiyo ya kisiasa kwa siku sitini. Mikutano itaruhusiwa kufanyika kwenye ukumbi pekee.

Muda wa katazo la kutoka nje kati ya saa nne usiku na saa kumi macheo litadumu hadi Januari 3 2021.

Maeneo ya Burudani na migahawa imetakiwa kufungwa kabla ya saa tatu usiku.

Wafanyakazi wa serikali walio na umri wa zaidi ya miaka 58 na wale walio na matatizo ya kiafya watafanya kazi wakiwa nyumbani.

Mikutano kati ya mawaziri, Makati wa kudumu na maafisa waandamizi wa serikali imepunguzwa, na mikutano yao itafanyika kwa njia ya video.

Wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mitihani ya kitaifa wakiwemo wa darasa la nane, kidato cha nne, wataendelea na masoko yao chini ya uangalizi wa kiafya.

Masomo kwa wanafunzi wengine yataendelea kwa njia ya internet na wanatarajiwa kurejea darasani kwa masomo ilivyokuwa kawaida, Januari mwaka 2021.

Safari kuingia na kutoka katika majimbo

Kulingana na rais Uhuru Kenyatta, safari kuingia na kutoka katika baadhi ya majimbo zitapigwa marufuku iwapo maambukizi yataendelea kuongezeka katika majimbo hayo.

Zaidi ya watu 58,000 wameambukizwa virusi vya Corona nchini Kenya kufikia sasa. Watu 1051 wamefariki.

Imetayarishwa na mwandishi wetu wa Nairobi Kennedy Wandera

XS
SM
MD
LG