Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:17

Dangote kujenga kiwanda cha kusafisha mafuta Nigeria


Aliko Dangote
Aliko Dangote

Tajiri mkubwa sana barani Afrika Aliko Dangote yuko kwenye mazungumzo na makampuni makubwa ya mafuta ulimwenguni, ikiwajuhudi ya kufadhili kiwanda cha kusafisha mafuta nchini Nigeria.

Kiwanda hicho kiko nje ya mji mkuu wa kibiashara wa Lagos, kulingana na vyanzo vinavyo fahamu suala hilo, ingawa kampuni yake imekanusha madai hayo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP kiwanda hicho kinachotarajiwa kutoa mapipa 650,000 kwa siku wakati kikimalizika, kitakua kikubwa zaidi barani humo, kikitarajiwa kubadili biashara ya mafuta ya kieneo.

Ingawa Nigeria ndiyo mzalishaji mkubwa zaidi pamoja na muuzaji wa mafuta barani Afrika, kwa kiasi kikubwa inategemea uagizaji wa bidhaa hiyo kutoka mataifa ya nje baada ya kuchakaa kwa kiwanda chake chenye uwezo wa kusafisha mapipa 445,000 kwa siku.

Viongozi wengi wa kisiasa akiwemo rais wa sasa Muhammadu Buhari wametangaza mpango wa kufufua kiwanda hicho lakini wakakosa ushirikiano wa kisiasa kutoka kwa viongozi. Kampuni ya Dangote inasemekana kuhitaji ufadhili wa kifedha ili kukamilisha mradi huo kutokana na athari zilizosababishwa na janga la corona pamoja na kupanda kwa gharama za ujenzi.

XS
SM
MD
LG