Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:31

California : Juhudi za kumuondoa Gavana Mdemokrat zagonga ukuta


Gavana wa California Gavin Newsom akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuibuka mshindi Jumanne, Sept. 14, 2021. (AP Photo…
Gavana wa California Gavin Newsom akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuibuka mshindi Jumanne, Sept. 14, 2021. (AP Photo…

Wapiga kura katika jimbo la magharibi la Marekani – California wamepinga juhudi za kumuondoa gavana wa Mdemocratic Gavin Newson madarakani.

Karibu asilimia 70 ya wapiga kura waliamua Newsom aendelee na kazi yake na kusema kuwa alishukuru na kuongea kwa unyenyekevu kuhusu kura hizo.

“Tunafurahia wingi mkubwa wa kura za hapana usiku wa leo hapa katika jimbo la California. Lakini hapana sio uamuzi wa pekee ulionyeshwa usiku wa leo. Nataka kulenga kile tulichosema Ndio kama jimbo."

Rais Joe Biden akiwa na Gavana wa California Gavin Newsom, na mkewe, Jennifer Siebel Newsom, wakiwasalimia wafuasi wa Chama cha Demokrat kabla ya uchaguzi ulioitishwa tena, Sept. 13, 2021, eneo la pwani, Long Beach California (AP...
Rais Joe Biden akiwa na Gavana wa California Gavin Newsom, na mkewe, Jennifer Siebel Newsom, wakiwasalimia wafuasi wa Chama cha Demokrat kabla ya uchaguzi ulioitishwa tena, Sept. 13, 2021, eneo la pwani, Long Beach California (AP...

"Tumesema ndiyo kwa sayansi, tumesema ndio kwa chanjo, tumesema ndio kumaliza janga. Tumesema ndio kwa haki ya watu kupiga kura bila kuwa na hofu ya kutokea ulaghai na ukandamizaji wa wapiga kura. Tumesema ndio kuhusu haki za msingi za wanawake kikatiba kuamua wenyewe nini anataka kufanya katika mwili wake, mwelekeo wake wa baadae. Tumesema ndio kwa mabadiliko. Tumesema ndio katika kujumuishwa,” wameeleza watu mbalimbali waliohojiwa," ameeleza Gavana Gavin Newsom.

Larry Elder
Larry Elder

Larry Elder mkonsevative na mwongozaji wa kipindi cha radio aliyekuwa mpinzani wa karibu wa Newsom amewasihi wafuasi wake kukubali kushindwa.

Wakati wa hotuba yake ya kukubali kushindwa alisema hawajapata ushindi lakini watashinda vita.

”Hebu angalia watu hawa wote, ikiwa Barack Obama, au Elizabeth Warren au Bernie Sanders. wote ambao walitoa matangazo kwa ajili ya Gavin Newsom, lakini hawajasema kamwe maneno haya. Gavin Newsom amefanya kazi nzuri kwa watu wa California. Ni warepublican wanaotaka kunyakua madaraka! Ni wazungu wenye itikadi za kibaguzi! Mkaribishe mtu mweusi kwenye itikadi kali za wazungu. Msicheke., msicheke nimefanya kazi kubwa kupata sifa hiyo,” ameeleza Elder.

Wachambuzi wanaeleza kama angeshindwa katika jimbo linaloshikiliwa na Wademokrati kungeweza kuashiria shida kubwa kwa Rais wa Marekani Joe Biden na wabunge wa chama cha Democrat kuelekea katika uchaguzi wa katikati ya awamu mwaka ujao.

XS
SM
MD
LG