Utawala huo uliomuondoa madarakani rais Alpha Konde umesema kwamba utashauriana na viongozi wa kisiasa, wafanyabiashara pamoja na viongozi wa kidini kwenye mji mkuu wa Conakry.
Ripoti zinaongeza kusema kwamba wanatumai viongozi hao watakubaliana kuhusu ni nani atakayeongoza serikali ya mpito pamoja na kufanyika kwa mageuzi ya kisiasa kabla ya kufanyika kwa uchaguzi.
Jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika magharibi ECOWAS, ambayo imesimamisha kwa muda uanachama wa Guinea imeomba kuundwa kwa serikali ya mpito ya kiraiya.
Wiki iliyopita kikosi maalum cha jeshi kikiongozwa na Mamady Doumbouya kiliipindua serikali baada ya maandamano ya muda mrefu ya wananchi waliokuwa wakilalamikia nia ya Conde ya kuwania urais kwa muhula wa tatu.
Mapinduzi hayo yamekaribishwa na mahasimu wa Conde akiwemo Cellou Dalien Diallo aliyekuwa waziri mkuu na ambaye ameshindwa kwenye uchaguzi wa rais mara tatu.