Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:50

Benki kuu ya dunia yaonya kuhusu janga la uhamiaji


 Viongozi kwenye mkutano wa awali wa kujadili mabadiliko ya hali ya hewa
Viongozi kwenye mkutano wa awali wa kujadili mabadiliko ya hali ya hewa

Ripoti iliyotolewa Jumatatu na Benki ya dunia inasema kwamba zaidi ya watu milioni 200 huenda wakalazimika kuondoka makwao katika kipindi cha miongo mitatu ijayo iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa ili kupunguza uchafuzi wa hewa pamoja na ukosefu wa usawa wa maendeleo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, ripoti hiyo ya Groundswell inaangazia athari zinazoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa, kama vile upungufu wa maji, upungufu wa uzalishaji chakula, ongezeko la maji baharini, masuala ambayo huenda yakasababisha uhamiaji wa mamilioni ya watu kufikia mwaka 2050.

Ripoti hiyo inasema takriban watu milioni 216 huenda wakalazimika kuhama makwao kwenye maeneo 6 ulimwenguni kutokana na uchafuzi wa hewa na ukosefu wa usawa wa kimaendeleo. Maeneo hayo ni pamoja na Latin Amerika, Afrika kaskazini, Mashariki mwa Ulaya na Asia ya kati, Asia kusini na Asia mashariki pamoja na eneo la Pacific.

Ripoti hiyo pia imeonya kwamba huenda kukajitokeza maeneo yenye misongamano mikubwa ya wahamiaji katika kipindi cha muongo mmoja, hali hiyo ikitabiriwa kudorora kufikia mwaka wa 2050.

XS
SM
MD
LG