Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 15:54

Kura ya kujaribu kumuondoa gavana wa California yafanyika


Picha inayoonyesha wapinzani wa gavana Gavin Newsom wa California wakipeperusha mabango ya kupinga uongozi wake.
Picha inayoonyesha wapinzani wa gavana Gavin Newsom wa California wakipeperusha mabango ya kupinga uongozi wake.

Kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha karibu miongo miwili, wapiga kura wa jimbo la California hapa Marekani Jumanne wanaamua ikiwa watamuondoa gavana wao, kupitia kura ya maoni ambayo pia inaambatana na uchaguzi.

Gavana Gavin Newsom anakabiliwa na upinzani kutoka kwa wagombea 46, na anahitaji angalau asili mia 50 ya kura ili kwendelea kuliongoza jimbo hilo kubwa zaidi nchini Marekani.

Swali la kwanza kwenye karatasi za kupiga kura ni iwapo mpiga kura anaunga mkono kuondolewa kwa gavana wa sasa wa chama cha Democratic Gavin Newsom.

Katika siku za karibuni, viongozi wa kitaifa wa chama chake wamekuwa wakitafakari utendakazi wake, katika kipindi cha miezi 20 iliyopita, huku baadhi wakiwarai wapiga kura kuendelea kuunga mkono uongozi wake kama gavana.

Rais Joe Biden alimpigia upatu Newsom Jumatatu usiku katika mji wa Long Beach akimwita mpinzani wa karibu zaidi wa Newsom, Larry Elder, "mtu anayefanana na rais wa zamani Donald Trump."

Wapinzani wa Newsom pia wameongeza kampeni zao katika siku za mwisho za uchaguzi huku utafiti wa maoni ukiashiria uwezekano mkubwa wa Newsom kukubaliwa kwendela na kazi yake.

Wakati kura zilipoanza kupigwa Jumanne mwendo wa saa mbili asubuhi, tayari idadi kubwa ya wakazi wa jimbo hilo, walikuwa wamepiga kura za awali kwa njia ya posta

XS
SM
MD
LG