Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:54

Waziri Mkuu wa Haiti amfuta kazi mwendesha mashtaka


Mwendesha mashtaka amshutumu Waziri Mkuu wa Haiti
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:02 0:00

Mwendesha mashtaka amshutumu Waziri Mkuu wa Haiti

Mzozo wa kisiasa wa Haiti umezidi kuwa mbaya baada ya Waziri Mkuu Ariel Henry, Jumanne kumfuta kazi mwendesha mashtaka wa umma.

Mwendesha mashtaka huyo alimshutumu Waziri Mkuu huyo kuwa alihusika katika mauaji ya Rais Jovenel Moise Julai saba.

Uamuzi wa Henry kumfuta kazi mwendesha mashtaka Bed Ford Claude umeweka wazi mapambano ya ndani ya ngazi ya juu kwa kile kilichobaki katika serikali ya Haiti zaidi ya miezi miwili baada ya Jovenel Moise kuuwawa kwa kupigwa risasi na watu waliovamia nyumba yake binafsi katika eneo la Porta Prince.

Claudie alifutwa kazi saa kadhaa baada ya kumuomba Jaji aliyekuwa anafanya uchunguzi wa mauaji ya Moise kumfungulia mashtaka Waziri Mkuu kwa kuhusika katika kesi hiyo.

Claude alisema wiki iliyopita rekodi za simu zinaonyesha kuwa Henry aliwasiliana mara mbili na mwanaume anayeaminika kuwa alikuwa mkuu wa mpango wa mauaji ya Moise usiku wakati uhalifu huo unatokea.

XS
SM
MD
LG