Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 09:20

Vurugu zaendelea Haiti siku kadhaa baada ya mauwaji ya Rais


Polisi wa Haiti wazingira washukiwa wa mauwaji ya rais Jovenel Moise
Polisi wa Haiti wazingira washukiwa wa mauwaji ya rais Jovenel Moise

Haiti Alhamis iligubikwa na vurugu  siku moja tu baada ya kuuwawa kwa rais Jovenel Moise.

Serikali imeapa kuwasaka watu wanaodaiwa kuwa mamluki na ambao walitekeleza uhaini huo, wakati akiwa kwenye chumba chake cha kulala.

Jumatano polisi walisema kuwa waliwaua washukiwa wanne wa shambulizi hilo kwenye mji mkuu wa Port au Prince, huku wengine wawili wakikamatwa. Maafisa watatu wa usalama waliokuwa wametekwa nyara na wauwaji hao pia waliachiliwa.

Mkuu wa polisi wa Haiti Leon Charles, amewaambia wanahabari Alhamis kwamba washukiwa wengine wanaendelea kusakwa. Kaimu waziri mkuu wa taifa hilo Claude Joseph muda mfupi baada ya tukio hilo alitangaza hali ya kijeshi,ikiwa na maana kwamba sheria za kijeshi zitatumika.

Amesema kuwa waliotekeleza ukatili kwenye taifa hilo masikini lenye idadi ya watu milioni 11,ni lazima wawajibishwe. Hata hivyo taarifa za kina kuhusu washukiwa waliouwawa bado hazijatolewa. Walichosema tu ni kwamba mauaji hayo yalitekelezwa na watu wenye utaalam mwingi.

XS
SM
MD
LG