Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 15:57

Waziri Mkuu wa Haiti aahidi familia ya rais aliyeuawa 'itapata haki'


Rais wa Haiti Jovenel Moise, katikati, akiwa na mkewe Martine Moise na Waziri Mkuu wa mpito Claude Joseph, kula, wakati wa maadhimisho ya uhuru wake Mei, 18, 2021.(AP Photo/Joseph Odelyn, File)
Rais wa Haiti Jovenel Moise, katikati, akiwa na mkewe Martine Moise na Waziri Mkuu wa mpito Claude Joseph, kula, wakati wa maadhimisho ya uhuru wake Mei, 18, 2021.(AP Photo/Joseph Odelyn, File)

Maafisa wa serikali ya Haiti wamewaomba wananchi kuwa watulivu wakati wanaendelea na uchunguzi kufuatia mauaji ya Rais wa nchi hiyo, Jovenel Moïse.

Waziri Mkuu Claude Joseph, alisema familia ya Moïse "itapata haki."

Polisi nchini humo wamesema kwamba kikosi cha watu 28 wakiwa pamoja na raia wa Marekani na Colombia walimuua Rais Moise na kuongeza kuwa wanane bado walikuwa hawajulikani waliko huku taifa hilo la karibian likitumbukia kwenye vurugu za kisiasa.

Nchi hiyo ambayo ni maskini sana katika ukanda wa Amerika kwa sasa haina rais wala bunge linalofanya kazi.

Pia amesema nchi hiyo hivi sasa ina watu wawili kila mmoja anadai kuwa ni waziri mkuu.

Jana Alhamisi polisi waliwaonyesha baadhi ya washukiwa mbele ya waandishi wa habari, pamoja na pasipoti za Colombia na silaha walizokuwa wamezikamata.

Washukiwa wanaohusishwa na mauaji ya Rais wa Haiti hayati Jovenel Moise
Washukiwa wanaohusishwa na mauaji ya Rais wa Haiti hayati Jovenel Moise

Mkuu wa idara ya Polisi ya Kitaifa ya Haiti, Leon Charles, aliapa kuwasaka na kuwatia mbaron wengine wanane waliotoweka.

Léon Charles, mkuu wa idara ya Polisi ya Kitaifa, Haiti amesema : Leo tuliwaonyesha wauaji hawa kwa wananchi. Walikuwa 26 na tuliwakamata 17. Kati yao ni Wakolombia 15 ambao tuliwatambua kwa hati zao za kusafiria; kuna Wamarekani wawili wa asili ya Haiti, ambao ni kati ya wale waliokamatwa.

Maafisa hata hivyo hawakuzungumzia sababu ya mauaji ya Rais Moise, wakisema tu kwamba shambulio hilo lililolaaniwa na vyama vikuu vya upinzani vya Haiti na jumuia ya kimataifa lilitekelezwa na "kikundi chenye mafunzo ya hali ya juu, na kilichokuwa na silaha nzito.

XS
SM
MD
LG